Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kuchangia katika bajeti hii ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mheshimiwa Spika, kwanza mimi badala ya kumpa hongera wifi yangu, Mheshimiwa Prof. Ndalichako, namna pole maana najua hapa kabeba mzigo mzito sana ambao ndiyo roho ya nchi yetu; nakupa pole sana.

Mheshimiwa Spika, na wakati nikiangalia kwa nini tumefikia hapa tulipofikia kwamba wanafunzi wetu anamaliza mpaka chuo kikuu anatembea na briefcase ya certificate kutafuta kazi; tatizo liko wapi. Nikaona niangalie maeneo mawili; la kwanza nimeangalia tulipoacha ile – sijui tunaita sera au nini – Mwalimu Nyerere alituweka katika njia ya kufikiria kwamba uhuru na kazi na pili, elimu ya kujitegemea. Nakumbuka elimu ya kujitegemea miaka hiyo nikiwa sekondari tulikuwa na mashamba kama ulivyokuwa unasema, tunalima tunapata chakula cha shule, lakini sasa hayo tumeyaacha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine nililoona tumekuwa donor dependent so much that hiyo imetulemaza. Hata Mheshimiwa wifi yangu Profesa akizungumza alitaja wafadhili au wadau wengi wanaotusaidia katika elimu yetu. Hii imetulemaza kiasi kwamba hatukutaka kujijengea njia ya kujitegemea wenyewe na kutafuta hela, badala yake tumetegemea sana wafadhili. Sehemu kubwa ya pesa ya maendeleo mfadhili asipoileta kwa wakati tunaanguka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapo natumia theory ya mtaalam mmoja Mmarekani anaitwa Ajzen na theory yake ya planned behavior, aliandika mwaka 1991. Alisema kwamba: “An individual attitude is shaped by subjective norms in the leaving environment and later such attitude forms intention within an individual and consequently this becomes a behavior”. Kwa Kiswahili ambacho labda siyo sahihi sana alisema: “Fikra ya mtu iliyojengwa na mazingira anayoishi humpelekea kuwa na nia ya kutenda kila kitu fulani na nia hiyo ikiendelezwa baada ya muda fulani hugeuka kuwa tabia”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini nasema hivyo? Sasa hivi tuliwajengea wanafunzi wetu kwamba akimaliza shule lazima aajiriwe, hiyo kuwatoka haijawa rahisi. Nataka tu-compare na nchi za wenzetu ambao walikuwa maskini au walikuwa wako nyuma wakati wakipata uhuru. Tanzania tukilinganisha na nchi ambayo ni ya China na Japan; nataka kuzitumia hizo maana najua hali zao zilikuwa duni wakati wakipata uhuru. Kwa mfano, tukipata uhuru sisi mwaka 61 China walikuwa wamepata uhuru wao mwaka 49 na Japan 51, tulipishana kama miaka kumi au kumi na miwili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia umri wa kuanzia masomo ya wanafunzi wao wa primary ni ile ile miaka sita kama sisi. Miundo yao ya elimu haijatofautiana sana na sisi, tunakuja kupishana sehemu moja au mbili. Sehemu moja uwiano wa walimu na mwanafunzi, hapo sasa hivi ndiyo tuna shida kubwa sana. Mwalimu mmoja wa Tanzania anakuwa na wanafunzi wengi kiasi kwamba hawezi kujua kila mwanafunzi ana karama gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Japan mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi 16.1, China 16.43, hii ni ripoti ya UNICEF siyo yangu sisi ni 50.63. Pia wameonyesha katika ripoti yao, ni ya siku za nyuma kidogo inawezekana mambo yamebadilika, wameonyesha kwamba wanafunzi wanaofaulu kwenda sekondari kwa Tanzania ni asilimia 54, Japan ni asilimia 98.8 na kwa China 97. What does that mean? Ina maana wao kwa vile ni compulsory na wanatumia ile system yao ambayo tangu primary school lazima wawe na vipindi vya ufundi na ufundi ule wanapewa equipment (vitendea kazi) kwamba hawa-relay kwenye nadharia kama sisi instead wao wanafanya kwa vitendo na zile product wanazotengeneza zinakuwa na value zinaenda hata kuuzwa.

Mheshimiwa Spika, hawa wanafunzi wakifika form four wengine wanakwenda kwenye shule za ufundi na wengine wanaenda shule za sekondari. Kiasi kwamba kama hakuweza kwenda chuo kikuu ameshajenga msingi na anajua aende akafanye kazi gani maana amepata zile skills. Kwa hiyo, zile skills zinawafanya wajenge tabia ya kujitegemea tofauti na sisi tunajenga tabia ya kwenda kuajiriwa.

Mheshimiwa Spika, wenzangu walikuwa wanasema tuwe na Baraza la Taifa la Elimu, lakini nafikiri hapo tutakuwa tumeji-confine sana, labda tuwe tunasema think tank ya kuangalia mfumo wetu mzima ambao utakuwa na linkage na viwanda, kilimo na Hazina kuona kwamba huu uchumi wetu na hasa shule zetu tunazi-revamp namna gani kusudi tujenge ile tabia ya kujitegemea. Kinyume cha hapo tutasema hatuja-improve hiki na hiki lakini wakijengewa tabia ya kujitegemea na tangu mwanzo tunaweka vifaa vya kutosha kwenye zile karakana na mwanafunzi akifika form four ameshajua anataka kwenda wapi. Hawa wenzetu hata university wana-liaise na viwanda, wanafanya attachment, wanakwenda kuona tunaweza kui-improve vipi viwanda vyetu au viwanda vinaweza kusaidiaje wale wanafunzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa kwetu sasa hivi tunafanya kazi kwa mtazamo mmoja, kama ni elimu tume-drawn a line ni elimu, kilimo ni kilimo. Sijui kama kuna mahali ambapo tuna-converge, tukitaka kuanzisha kiwanda lazima tuangalie skills gani tunawapa wanafunzi wetu, kwa priority ipi na kwa viwanda vipi. Bila kuweka huo muelewano kwamba hawa wa viwanda wanajua priority ya viwanda vyetu ni hizi, kwa hiyo tunapoweka mitaala yetu tunalenga kwamba wanafunzi wetu lazima wafundishwe au wapitie huku wajue kwamba tunalenga kwenye viwanda hivi.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano, pamba sasa hivi bado pamba tunapeleka nchi za nje tuna-create employment kwa wenzetu. Tunanunua mitumba au tunanunua nguo kwa bei mbaya. Baada ya kufanya kazi na hawa wenzetu donors wanapenda tuwe donor depended so much that tusiweze kujitegemea maana once tumeweza kujitegemea hawataweza kupata raw materials waka-create employment kwao. Ndiyo maana wakija wanakuja na watu wao wenye skills. Sisi tunasema ooh wale ambao hatuna mje nao kwa nini sisi hatu-train watu wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nafikiria kama alivyokuwa anasema Mheshimiwa Kimei pale walimu wetu wapelekwe nje wapate exposure, short of that tutakuwa hatufiki mbali. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante.

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)