Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kipee wewe mwenyewe binafsi, kwa kunipa nafasi hii lakini nitumie nafasi hii kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wanamichezo kwa heshima kubwa walionipa ya kunichagua kuwa Mwenyekiti wa Bunge Sports Club tena katika uchaguzi ambao kwa bahati mbaya sana sikuwepo, hivyo nilichaguliwa nikiwa sipo nataka niwaambie kwamba nitarudishia hisani hiyo kwa kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mchango wangu naupeleka kwenye masuala ya barabara, nimekuwa nikiangalia kila Mheshimiwa Mbunge anayesimama karibu asilimia zaidi ya 80 ya sisi tuliomo humu ndani tumekuwa tukizungumzia suala la TARURA. TARURA ni chombo kipya chombo ambacho tumekipa majukumu makubwa sana zaidi ya mzigo wanaoweza kuubeba. Wenyewe hawana chanzo cha fedha zaidi ya allocation ambayo Serikali inawapa kupitia road fund.

Mheshimiwa Spika, wanamtandao wa zaidi ya kilomita laki 100 na katika hizo kilomita zaidi ya 78,000 zote ni mbaya, unategemea nini katika utaratibu tunaotaka kwenda nao wa kuinua tija na kuinua mapato kwa wananchi wetu kuinua uchumi katika nchi ambayo barabara nyingi kwa mujibu wa hotuba ya Mheshimiwa Waziri ni barabara mbaya unapata wapi tija na uchumi ukakuwa kwa kasi tunayoitaka si rahisi.

Mheshimiwa Spika, na ubaya utakuta kwamba TARURA yenyewe kwa kuwa ipoipo natumia neno ipoipo kwasababu haijakuwa intergrated na mifumo ya kisheria iliyopo katika nchi hii. Nawapa mfano mmoja ukiangalia sheria ya Urban Planning Act ile ya mwaka 2007, hasa section seven ambayo inatoa mamlaka ya upangaji wa miji, kwa mamlaka za city, municipal, ama za mjini. Lakini TARURA inakuja inafanya maamuzi yake ya kujenga barabara vile wanavyotaka wao hakuna consultation kati ya TARURA na urban authorities ama planning authorities na hiyo inatupa matatizo makubwa kwasababu user ni wananchi wa maeneo husika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano pale Kinondoni, utakuta kwamba Kinondoni tuko mjini lakini ukienda kwenye kata zote hali ni mbaya sana katika sana katika barabara. Ukienda Kigogo hali mbaya, ukienda Mwananyamala angalau kidogo ukienda Makumbusho ukienda wapi unamleta Manager wa TARURA kwa mfano anatoka Kigoma kwa wakwe zangu kule unamleta Kinondoni hajui mahitaji ya Kinondoni na hafanyi consultations na urban authorities unatarajia nini.

Mheshimiwa Spika, na hii ndio unaikuta katika maeneo mengine kwamba kwa kuwa hakuna consultations na wao ndio wanaojenga barabara tunapata matatizo na matatizo hayo yanapeleka kwa mfano kule Kinondoni sisi si wakulima hatuna bahari hatuvui pale katika Jimbo la Kinondoni kazi yetu sisi ni biashara na uchuuzi na shughuli nyingine ndogondogo tunahitaji kutembea sana, tunahitaji barabara ambazo ziko nzuri ambazo zinapitika. Sasa ukiangalia pale kwetu utakuta tunahitaji moja kubwa la barabara ambayo ni kilomita tatu tu iko kuanzia pale Mtaa wa Mlandizi kule na inakuja inapita sehemu za makumbusho inakwenda kuhudumia, kata karibu nne.

Mheshimiwa Spika, sasa ningemuomba Mheshimiwa Waziri kwamba apate muda yeye ama wasaidizi wake twende nao Kinondoni wakaangalie pamoja na kwamba Kinondoni ndio Dar es Salaam, lakini hali ni mbaya sana za barabara na hasa mvua zinaponyesha tunakuwa na adha kubwa sana na ukiangalia Wananchi wa Kinondoni ni moja kati ya watu ambao wanachangia sana katika kodi za Serikali ikiwemo mapato ya pale Kinondoni kwenyewe ambako tunakusanya zaidi ya bilioni 40 kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na hili ningeiomba Serikali sasa iweze ohh! my God! naunga mkono hoja. (Makofi)