Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Hon. Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Msingi wa kujenga uchumi wa viwanda ni kuwa na technical schools au colleges, niipongeze Serikali kwa kuboresha baadhi ya vyuo hivyo, yaani sekondari za ufundi chache katika nchi hii, angalau wameboresha majengo. Sasa niombe licha ya kuboresha majengo hayo, waboreshe na vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji, kwa sababu, majengo tu hayatasaidia.

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge wenzangu wanajua kwamba zile shule zilikuwa zinasikika sana; Ifunda, Iyunga, Mtwara, Moshi Technical, hizi sekondari sasa hivi hazisikiki kwa sababu ubora umepungua. Kwa hiyo, niwaombe sana Serikali waziangalie, majengo pamoja na vifaa vya ufundishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika ufundishaji waboreshe kwa kutumia Taasisi ya Elimu ili waweze kuwapa mafunzo wale Walimu ya ufundishaji mahiri, tunaita competent base, tumeizungumza sana hiyo toka 2005, lakini ni practice bado Walimu wanafundisha kwa kuwajaza wanafunzi maarifa, wanawajaza, wanawajaza, lakini practical skills zimewekwa pembeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nirudi kwa watendaji. Ni kweli kuna baadhi ya watendaji wetu wanatuangusha, lakini kuna baadhi ya Wakurugenzi wanafanya kazi vizuri, wakati wote tunaangalia wale wanaofanya vibaya, lakini wapo wazuri. Hivyo, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, wapewe pongezi zao, wapewe recognition. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna Mkurugenzi alikuwa anafanya kazi pale Jiji, nitoe mfano, wakati anakuja pale, maegesho tu walikuwa wanapata milioni 84 kwa mwezi, lakini alipoingia yeye akakusanya bilioni 1.6 kwa mwezi. Wakurugenzi kama hao naomba wapewe recognition, Maslow’s hierarchy inasema binadamu siyo fedha tu, binadamu siyo mapenzi tu, binadamu siyo shughuli nyingine, binadamu hata kule kutambuliwa anaweza akafurahi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa stendi ya Mbezi huyo Mkurugenzi aliweza kuokoa bilioni zaidi ya 12. Hizo zingepigwa, kwa hiyo, hapa nimesimama kuzungumzia kwamba Wakurugenzi wengine ni kweli siyo mahiri, lakini kuna wale wazuri tuwatambue na wapewe recognition. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho, nizungumze kwa watumishi; tunapozungumza ni watumishi na wengi zao ni Walimu, tunasema Walimu ndiyo wengi katika watumishi, kwa hiyo, tunapowatetea Walimu na mimi ni mwalimu, tunapowatetea siyo kwamba watumishi wengine tumewaacha pembeni.

Mheshimiwa Spika, Walimu wanafanya kazi nyingi mno na sisi ni mashahidi, tukija uchaguzi Walimu, tukija kwenye sensa tunategemea Walimu, watoto wetu tumewaacha mashuleni huko Walimu. Jana nilikuwa na Mheshimiwa mmoja akawa anasema jamani hawa Walimu wana kazi, sisi tuko huku watoto wako mashuleni huko. Kwa hiyo, tunapotetea wapandishwe mishahara, ni kwa sababu ndiyo kundi kubwa na limeshasemwa siku nyingi, lakini bado walimu mishahara yao hairidhishi, licha ya matatizo yao mengi ambayo wanakuwa nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nikushukuru sana. (Makofi)