Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu

Hon. Twaha Ally Mpembenwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibiti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi kuwa mchangiaji wa kihistoria leo kwa kuwa mchangiaji wa kwanza katika session hii ya jioni.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, nichukue fursa hii kwanza kabisa kuipongeza Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa uwasilishaji mzuri. Kwa kweli hotuba hii imetupa dira nzuri ya kuonyesha kama Serikali wapi tulikotoka, nini kimefanyika na yale ambayo tunakusudia kwenda kuyafanya katika kipindi kijacho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi leo sitakuwa mzungumzaji wa mambo mengi sana, lakini nataka niguse tu katika maeneo kadhaa hasa katika miradi mikubwa ambayo Serikali wameweza kuitekeleza na wanakusudia kuitekeleza. Baada ya hapo, nitagusia kidogo mambo mawili, matatu katika jimbo langu.

Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na wazungumzaji wengine kusema kwamba ni ukweli uliokuwa wazi kwamba legacy aliyoiacha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli itakuwa inaenda kujieleza yenyewe. Kwa tafsiri hiyohiyo, ni matumaini yangu kuwa tunategemea kuanza kuona legacy mpya ya mama yetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hasa katika kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ambayo imeachwa na predecessor wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu niguse miradi ya kimkakati, kwa mfano mradi wa SGR, ni muhimu sana kwani unakwenda kufanya total transformation ya social economic transformation katika nchi yetu. Especially katika maeneo yote yale ambayo yatakuwa yanapitiwa na mradi ule, tunategemea kwa namna moja ama nyingine kutakuwa na mabadiliko makubwa sana ya kijamii na kiuchumi vilevile. Hivyo, ni mategemeo yangu kuona Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan wanakwenda kukamilisha miradi hii. Hii itatuwezesha sisi kama Serikali au kama Taifa kuwa na mapato ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, naomba vilevile nizungumzie mradi mzuri sana wa ndege. Mradi huu wengi sana wamejaribu kuongeaongea na wale rafiki zetu wengine ambao wako form six, walio-graduate kule marafiki zangu, waliweza kuzungumza mengi sana katika mradi huu. Nataka niseme tu mradi huu mama yetu ameanza vizuri sana, alianza kwa salam nzuri ya kuwasalimia Watanzania, kwa kusema nawasalimu Watanzania kwa salaam ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alisema kazi inaendelea katika majibu hayo. Katika majibu hayo mama ameanza vizuri, tayari yale malipo ya ndege tatu yameshakamilika, hivyo tunategemea kwenda kuona ndege nyingine zinaongezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirudie tena katika jambo hili la mambo ya ndege. Katika sekta nzima ya mambo ya aviation, sekta hii siku zote tafsiri yake pana ni kwamba inakwenda kuchochea uchumi wa nchi. Tunavyokuwa na National Flag Carrier maana yake ni kwamba tunakwenda kuitangaza nchi. Hivyo basi, niseme tu kama Serikali wamefanya jambo la busara na Mheshimiwa Rais alivyoweza kuzilipa ndege hizi tunakwenda kuona sasa mabadiliko makubwa yanakwenda kupatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niwatoe shaka Wabunge wenzangu, lakini vilevile na Watanzania kwa ujumla, kale ka-hasara kalivyokuwa kamezungumziwa, najaribu ku-refer kule katika Ripoti ya CAG isije sana ikatuumiza vichwa. Wenzetu Kenya mwaka jana waliweza kutengeneza loss ya Dola milioni 338; mwaka 2019 walitengeneza loss ya Dola milioni 258; mwaka 2018 walitengeneza loss ya Dola milioni 100 lakini bado wako stable, tafsiri yake ni kwamba wanafanya vizuri katika sekta tourism.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niweke ufahamu vizuri hapa kwa Watanzania pamoja na wale Wabunge wenzangu ambao ni form six. Tafsiri yake ni kwamba katika accounts kuna kitu kinaitwa net off maana yake ni kwamba kama kuna hasara inapatikana katika sekta moja inakwenda kuwa compensated katika sekta nyingine. Sisi kama Tanzania tumefanya vizuri na maono mapana ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kuimarisha suala zima la tourism. Hivyo, naiomba Serikali, twendeni tukapambane ili tuweze kuhakikisha tunakwenda ku-boost internal tourism ili sasa ndege zetu hizi zilizopatikana ziende kufanya vizuri kama kwa neighbor zetu wa Kenya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie mradi wa hydroelectric power. Nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, alikwenda katika eneo ambapo mradi ule unafanyika, maelezo aliyoyatoa ni ya faraja na ya kuwatia matumaini hasa Watanzania na vilevile wajomba zangu wa Rufiji na sisi watu Kibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu unafanyika katika maeneo makubwa mawili, kuna upper stream na downstream. Sisi tupo kule katika maeneo ya downstream, kuna hekari takribani 150,000, napenda sana kuiona Serikali sasa inakwenda kujielekeza katika mradi ule ili sisi watu wa Kibiti na Rufiji tuweze kunufaika katika masuala mazima ya umwagiliaji. Kilimo cha umwagiliaji ni cha msingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu unavyokwenda kukamilika na tumeambiwa kwamba fedha zipo na mimi sina shida na sina shaka na Serikali ya Awamu ya Sita najua fedha zipo na mengi yameshaanza kufanyika. Ni imani yangu kwamba tutakwenda kuwa na mradi wa umwagiliaji ili tuweze kuhakikisha mradi huu ya hydroelectric power unakwenda sambamba na mradi na mradi ule wa umwagiliaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee sasa mambo yangu ya jimboni. Nimshukuru tu Mheshimiwa Rais ameanza vizuri, kama alivyoanza kusema kwamba kazi inaendelea, ni kweli kazi inaendelea. Hivi ninavyoongea tayari shilingi milioni 594 zimeshapelekwa katika kumalizia jengo la Mheshimiwa Mkurugenzi wetu wa Wilaya. Sambamba na hilo tumeweza kupewa fedha takribani shilingi milioni 500 tunakwenda kujenga wodi tatu katika Hospitali ya Wilaya. Tumepewa fedha nyingine shilingi milioni 180 katika kukamilisha maabara 6. Fedha hizi zimepatikana kutokana na mama huyu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama hiyo haitoshi, tumeweza kupewa fedha nyingine takribani shilingi milioni 136 katika mradi wa maji. Hivi navyozungumza tayari katika Kata ya Dimani maji yanatoka, mambo yetu yanakwenda bambam. Nani kama mama?

WABUNGE FULANI: Hakuna.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, mama huyu ameyafanya mambo mazuri na sisi ni mategemeo yetu anakwenda kuyafanya mazuri zaidi katika kuhakikisha kwamba kauli yake inayosema kazi inaendelea ni kweli kazi inaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya it’s not a rocket science, ni vitu ambavyo viko wazi, tayari tumeshalipa ndege tatu nani kama mama?

WABUNGE FULANI: Hakuna.

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, imani yangu kubwa Zaidi ni kwamba mama yetu Samia Suluhu Hassan anakwenda kutengeneza legacy nyingine ambayo ameiacha predecessor wake ya kukamilisha miradi mikubwa hii ya SGR na Hydroelectrical power na mingine kama nilivyokuwa nimezungumza. Kama hiyo haitoshi ametuambia Mheshimiwa Ummy Mwalimu hapa tunakwenda vilevile kujenga Vituo vya Afya katika wilaya zile ambazo bado hazijafikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima na unyenyekevu wa hali ya juu kabisa, napenda kusema naunga mkono hoja. Tumuombee mama yetu ili aweze kutusogeza mbele. Ahsante sana. (Makofi)