Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

Hon. Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi hii na mimi niweze kutoa mchango wangu kwenye hoja iliyoko mbele ya Bunge letu tukufu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wananizonga nyuma hapa, lakini naomba niendelee kwa sababu kama ulivyotueleza kama Kiti kwamba mamlaka zitatoa taarifa rasmi, sasa naomba Waheshimiwa Wabunge tuvumiliane kwa sababu mamlaka hizi zinatoka kwake na lazima tuziheshimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma mpango ambao unatuelekeza mpango wa mwaka mmoja lakini pia mpango wa miaka mitano na ninaomba nitoe mchango wangu katika eneo dogo la sekta ya afya, hasa kwenye eneo zima la uwekezaji katika sekta hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge awamu iliyopita nikiwa Mjumbe katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali tulitembelea Medical Stores Department (MSD) na kuona namna ambavyo wanafanyakazi, lakini wakati tuko pale kukawa na delegation kutoka nchi za SADC ambayo imekuja kufanya uchunguzi ili kuweza kuwapa MSD jukumu la kusambaza dawa katika nchi 16 za Kusini mwa Afrika (SADC), lakini tulijiridhisha kwamba kwa Sheria ya Uanzishwaji wa MSD walikuwa hawana mamlaka ya kuzalisha dawa isipokuwa ni kununua na kusambaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nimeleta hoja hii? Nimeileta kwa sababu dawa za binadamu zinazozalishwa hapa nchini ni asilimia nne peke yake katika dawa asilimia 100 ambazo tunazitumia. Ni asilimia nne tu ya dawa ndiyo zinazalishwa nchini; dawa nyingine zote tunazinunua kutoka nje ama Ujerumani au India. Sasa hoja yangu ni kwamba Wizara inayohusika na uwekezaji ni wakati mwafaka sasa kuhakikisha kwamba inavutia wawekezaji katika sekta hii ya dawa za binadamu ili kama tutapata soko la usambazaji wa dawa katika SADC dawa hizi ziwe zinatoka hapa hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, Wizara ya Afya iweze kuleta muswada Bungeni wa kuweza kubadilisha sheria iliyoanzisha Mamlaka ya MSD ili sasa iweze kuzalisha, lakini pia kusambaza kwa maana kwamba dawa zikiwa zinazalishwa hapa nchini itakuwa rahisi hata kuzisambaza katika hizi nchi za SADC tuweze kupata uwezo wa kwamba dawa zitakuwa zinazalishwa ndani ya nchi, lakini pia kwa kuwa MSD inaweza ikawa ndiyo msambazaji katika nchi za Kusini mwa Afrika basi tukapata multiplier effect kwenye uchumi wetu kwa mana ya uzalishaji na usambazaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo lingine ambalo ninataka kuchangia ni eneo la bandari; kwamba bandari yetu ni hub ya kiuchumi kwa nchi za Kusini mwa Afrika. Tunaomba iendelee kuboreshwa kwa maana kwamba kuweza kushindana na bandari nyingine zilizoko Kusini mwa Afrika hasa ile ya Beira na ya Johannesburg, Cape Town lakini pia na bandari ya kule Angola.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanini nazungumza hivi? Ni kwa sababu sisi tuko katika Ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo tunakumbana na changamoto za protocol mbalimbali za Afrika Mashariki, lakini wakati mwingine hizi protocol hazigusi Kusini mwa Afrika. Kwa hiyo, ni lazima tuwe makini sana pindi tunaposaini protocol za Ukanda wa Bahari wa Afrika Mashariki, tuzingatie kwamba sisi soko letu kubwa tumelielekeza Kusini mwa Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine na la mwisho ambalo ninapenda kutoa mchango ni eneo la viwanja vya ndege; gharama za kutuana gharama za ku-park katika viwanja vyetu vya ndege bado ni kubwa. Kwahiyoili kuwezesha mamlaka hizi za viwanja tuweze kupokea ndege nyingi kwa wakati mmoja, ni lazima tutazame eneo hili la Mamlaka za Viwanja vya Ndege kwa maana ya landing fees na parking fees ili ziweze kushawishi ndege za mashirika mbalimbali kuweza kutua hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nakushukuru kwa nafasi. (Makofi)