Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

Hon. Fakharia Shomar Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Mwenykiti, ahsante. Sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwenye kuumba mbingu na ardhi, vilevile kukushukuru na wewe Mwenyekiti ambaye ndio Naibu Spika na Mheshimiwa Spika na uongozi wote wa Bunge pamoja na Waziri Dkt. Mpango kwa huu Mpango wake uliokuwa mzuri, bora na uliotukuka, pamoja na Chama changu Cha Mapinduzi kilichoniwezesha kufika hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitazungumzia kidogo ukuaji wa pato la Taifa ambalo limeendelea hadi kufikia 6.9 na vile kufika katika kundi la uchumi wa kati. Kwa kweli ni jambo jema na jambo kama hili linataka kupigiwa upatu kila leo ili wale waliokuwa hawasikii wasikie na wale waliojifanya hawaoni, waone na wajue kwamba tuko vingine sisi Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuelezea pia mkakati uliokuwa umewekwa na Taifa ambao ni mkakati mkubwa, kwa mfano, ujenzi wa reli ya kati kiwango cha standard gauge; mradi wa kufua umeme wa maji; uboreshaji wa mashirika ya ndege; ujenzi wa barabara na madaraja, ni jambo la faraja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna deni kubwa hapa, tuko Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi, lakini hatuna uwanja wa ndege wa kuridhisha na uwanja wa ndege ndio unaoleta maendeleo ya nchi, Kiwanja kipo miaka 15 nyuma, lakini bado tunang’ang’ana na kiwanja kidogo, kiko katikati ya mitaa ya watu, sasa hili Mheshimiwa Dkt. Mpango aliangalie, nini tatizo wakati hapa ni Makao Makuu ya Mji na mikoa mingi imepakana? Kuna mikoa mingine haina viwanja vya ndege itakuwa rahisi wakitua Dodoma wakaweza kufika katika mikoa yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hilo nataka katika mipango yetu tunayopanga, mpango ni mzuri lakini unakuwa na upungufu mdogo mdogo ambao tuukumbuke ili tuweze kuushughulikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ambaye katika ukurasa wake wa 31 alielezea elimu stadi kazi za ufundi wa vijana wakimaliza elimu waweze kujiajiri; hili nimelikubali mia kwa mia. Elimu yetu kwa kweli tunaosomeshwa school ni ya kukariri ili upate shahada, ukimaliza kama umepata degree umepata Master ndio umemaliza, lakini kama utampa elimu stadi ya ufundi, akimaliza anajua anakwenda kufanya nini. Kijana huyu hata kama atakuwa ni fundi cherehani, lakini anajua nikiondoka nakwenda kufanya kazi fulani, kama nitakwenda kutengeneza baiskeli au kutengeneza magari. Hayo yote tunayafanya mtu aende ajibagize bagize kwenye magari mabovu afundishwe, lakini kama atapata toka school itamsaidia na ajira zitakuwepo, hatutoweza kutegemea ajira ya Serikali kwa sote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wale vijana watakaobahatika, watabahatika na tutakaobakia tutafanya kazi zetu wenyewe za kuzalisha mali kwa kufanya kazi nyingine hata kama kutakuwa na viwanda, wakati mtu unampeleka kiwandani, hana stadi ya elimu anaenda kufanya nini? Ina maana itakuwa umempeleka mahali akaanze kufundishwa, ambapo kile atakachofundishwa atakuwa shambaganga tu lakini sio uwezo wa kufanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye uchumi wa blue, uchumi wa blue ambao tunaiongelea bahari na bahari ina mazao mengi na bahari kuna wazee wetu wanafanya kazi kwa kutumia urithi wa babu, baba na mjomba, lakini haijui vipi bahari ilivyo. Sasa ningeshauri elimu ya bahari ingeanza kufundishwa kuanzia elimu ya msingi mpaka tunamaliza vyuo, unamjua mtoto ushampanga, anaijua bahari ikoje na anajua mazao ya bahari yanapatikana wapi. Sasa Serikali wakati itakapojitahidi kutafuta vifaa na watoto wameshasomeshwa, wanajua nini wanachokifanya, litakuwa ni jambo jema, ina maana tutaitendea haki blue economy na kila mmoja atajua anachokifanya. Ushauri wangu napenda masomo ya uchumi wa bluu wasomeshwe vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machache, naunga mkono hoja. (Makofi)