Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Silafu Jumbe Maufi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa uhai wake na afya njema kwangu na kuniwezesha kutoa huu mchango wangu kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu na wafuasi wote ndani ya Wizara hii. Mwenyezi Mungu awape afya na kuendelea vema ndani ya uwajibikaji uliotukuka ndani ya majukumu yao. Hakika umahiri wao ni makini kwa wananchi wetu na matokeo chanya yenye tija yanaonekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuzungumzia suala la zima la kilimo ambalo linawashirikisha karibu asilimia 75 ya wananchi wetu nchini. Tulikuwa na mikoa iliyokuwa ya uzalishaji wa mazao (mahindi) ya ziada na kuwa na big four lakini sasa nje na mwelekeo, kutokana na gharama ya pembejeo na mbolea kuwa kubwa na kuwapa changamoto wakulima. Pembejeo na mbolea kutofika kwa wakati kwenye maeneo, pembejeo na mbolea kuwa na bei kubwa. Changamoto hizi zinapelekea wakulima kurudi nyuma kwenye uzalishaji wa ubora wa mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa uzalishaji wao tunashauri Serikali yetu kujenga Kiwanda cha Mbolea na kuchanganya pembejeo ndani ya Mkoa wa Rukwa, tuweze kupunguza gharama kwa wakulima wetu ili waweze kurejea kwenye big four na hatimaye tuondokane na upungufu wa chakula hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, hakika bajeti ya mwaka huu, nitofautiane na bajeti zilizopita kwa vyanzo vilivyobainishwa kwa makusanyo ya mapato kwa maendeleo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kushauri Serikali yangu katika kuongeza mapato ukurasa 43 - 44. Bado nchi yetu tuna upungufu sana na mkubwa katika usambazaji wa maji kwa wananchi wetu hasa vijijini, hata vilivyo karibu na mito, maziwa na bahari. Mapendekezo ya asilimia 10 kwa vifaa vya plastiki vinavyohusika na miundombinu ya maji. Ushauri wangu ni bidhaa zinazozalishwa nchini zenye ubora kuwa 0% na bidhaa zitokazo nje ya nchi iwe 10%.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kushauri kuhusu ushauri wa vifaa bandia vya urembo kwa wanawake na wanaume kutokana na kupelekea kututoa kwenye uhalisia wa Utanzania wetu, ni bora ushuru kuwa ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, vitengenezavyo ndani ya nchi kuwa 25% na kutoa nje 35%. Tukiona huruma tujue wazi kuwa uhalisia wa wananchi wetu wa Utanzania utatoweka.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuongeza jitihada ya Serikali ya kuunganisha nchi za jirani, mkoa na mikoa, wilaya na wilaya ambayo ni hali halisi inayoendelea katika ukamilifu wake na kurahisisha wafanyabiashara kuchukua mazao kwa wakulima na kupeleka sokoni ambako wanapata kipato cha juu na kizuri ambacho kingekuwa vema kupatikana na wakulima. Hivyo nashauri Serikali kuona umuhimu sasa wa kuangalia vinginevyo na kuwapangia bajeti kuweka miundombinu ya kupitika mwaka mzima (masika hadi kiangazi) na kuunganisha vitongoji na vijiji na kata ambako ndiko kwenye mashamba ya uzalishaji ili wakulima wapate wepesi wa kufikisha mazao yao sokoni kwa urahisi na kuongeza vipato vyao kuliko kuwapa nguvu zaidi wafanyabiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kushauri kwa msisitizo kuhusu na kuifanyia usanifu barabara ya Kibaoni – Kiliyamatundu - Miangalua na kukutana na barabara kuu ya Tunduma - Sumbawanga kuwa ya lami kwani daraja kubwa la Momba ni lenye thamani kubwa lakini linaunganishwa na barabara za vumbi sio sahihi na hatutokuwa tunalitendea haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukurasa wa 38; nashukuru kwa kazi nzuri na pongezi ya jitihada kwa Serikali katika kuwaunga mkono wananchi kwa nguvu wazitoazo kwenye maendeleo ya kujenga miundombinu ya afya, elimu kwenye maeneo yetu na kuamua kutenga bajeti ya bilioni 271.33 za kukamilisha maboma kwa 2018/2019. Hata hivyo, bado maboma yanaendelea kwani kuna baadhi ya shule za msingi, sekondari, zahanati na vituo vya afya kwa asilimia ndogo waliokamilisha miundombinu katika ukamilifu wake. Pesa itoke kwa ukamilifu ili haya maboma 144 kwenye halmashauri zetu yakamilishwe. Bajeti hii ya 2019/2020 tuiboreshe na kuisimamia kutoka kwa wakati kwani maboma bado ni endelevu kutokana na elimu bure, ambayo ni faida kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.