Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara kwa kazi nzuri na yenye matumani. Nawatia moyo wasikatishwe tama, wakaze moyo ila watende haki na Mungu atakuwa nao.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri; katika umeme Wilaya ya Bukoba Vijijini kuna maeneo mengi sana hawajapatiwa umeme na Serikali inasema ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote vitakuwa vimeingiziwa umeme wa REA III. Kutokana na utekelezaji wa utaratibu kwa mradi inaweza ikamalizika bila umeme kufika, kwa hivyo ni vigumu viwanda kufanya kama wanavyosema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo; nashauri kuna wakulima wadogo wadogo wa miwa lakini wananung’unika malipo wanayolipwa katika Kiwanda cha Kagera Sugar ni kidogo sana, kuwepo na mfumo maalum wa kuwatetea waweze kulipwa malipo ya haki sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, maji; Mkoa wa Kagera Ziwa Victoria limechukua sehemu kubwa karibu wilaya zote, lakini ni manispaa pekee ndiyo haina shida ya maji, wilaya zilizobaki maji ya Victoria wanayaona tu, Serikali ijitahidi wilaya zote zisambaziwe maji kwa sababu ziko katika mkoa huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri mwingine; Sheria ya Kodi, Sura 332; kodi ya taulo za kike zitolewe bure kusudi wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waweze kujihifadhi pindi wawapo kwenye hedhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, nawatakia kazi njema katika kazi zao na Mungu awaongoze tena vizuri.