Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Mwanne Ismail Mchemba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Mpango, Waziri wa Fedha; Naibu Waziri, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji; Katibu Mkuu na Wizara yote ya Fedha kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kutumikia na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2025.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono kufuta kodi ya ongezeko la thamani kwa taulo za kike kwani hata mimi ni shuhuda wakati nanunua taulo hizo wakati napeleka shuleni, nilinunua kwa bei ya juu sana mwezi Agosti, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono kutoza ushuru wa nywele za kike ambazo zinatoka nje ya nchi na viwanda vya ndani pia. Ushuhuda wangu ni kwamba, nywele za nje huuzwa mpaka Sh.600,000 hasa za maharusi. Kwa nywele za viwanda vya ndani huuzwa mpaka Sh.30,000 kwa moja, niombe Serikali isirudi nyuma kwa mipango mizuri 2019/2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, TRA Dodoma ifuatilie maduka ya jumla, vituo vya mafuta ukusanyaji wake uko chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, afya; niombe Serikali ujenzi wa vituo vya afya vikikamilika ni vema vifaa tiba vipelekwe kwa wakati na watumishi wa afya wapelekwe haraka kwa kutengewa fedha.