Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Mbaraka Kitwana Dau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa fursa hii, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa kuwasilisha bajeti vizuri na yenye kuleta matumaini kwa Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza sana Serikali chini ya Rais wetu mpenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wenye maslahi mapana ya nchi wa kusitisha mchakato wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Ni ukweli usio na shaka mkataba ule haukuwa na maslahi na nchi yetu na ulikuwa unaelekea kuifilisi nchi. Hata hivyo, ujenzi wa bandari umuhimu wake bado upo pale pale, nichukue fursa hii kuiomba Serikali yangu sikivu ama kujadiliana upya na wawekezaji hawa au kutafuta wawekezaji wengine kwani kimsingi ujenzi wa reli ya kisasa SGR unategemea zaidi bandari kubwa kama ya Bagamoyo kusafirisha mizigo ili kuwezesha reli yetu ya kisasa kuweza kulipa gharama za mwekezaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa kielelezo wa ufuaji wa umeme wa nguvu za maji wa Stiegler’s Gorge ni mradi mzuri na naipongeza Serikali yangu kwa kutekeleza mradi huu uliobuniwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere. Sambamba na mradi, nashauri Serikali yangu kuanza utekelezaji wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mto Rufiji. Ni muhimu sana mradi huu ukaanza sanjari na ujenzi wa bwawa la kufua umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni mapato yatokanayo na watalii; hapa nazungumzia utalii katika Kisiwa cha Mafia. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Serikali, Kisiwa cha Mafia kinapokea watalii zaidi ya 5,000 kwa mwaka. Kwa kuzingatia ukweli na ukweli miundombinu ya usafiri ya kuingia na kutoka. Mafia haipitiki kirahisi ikiwemo upatikanaji wa boti ya kisasa na uwezekano wa Shirika la Ndege la ATCL kuanza safari zake katika Kisiwa cha Mafia. Nalileta hili ili Mheshimiwa Waziri kwa kushirikiana na Wizara ya Kisekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano washirikiane ili kuweza kutatua changamoto hizi na Kisiwa cha Mafia kiweze kufikika kirahisi na watalii wakaongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, uvuvi katika bahari kuu umesimama kwa takribani miaka mitatu sasa kutokana na changamoto ya tozo (royalty) ya dola 0.4 kwa kila kilo moja ya samaki aina ya Jodari (Tuna). Kwa kuwa meli hizi haziji kuvua na Serikali inakosa mapato kutokana na tozo ya kukata leseni, naishauri Serikali yangu kulitafutia ufumbuzi haraka sana jambo hili kwani samaki wanahama, wanazaliana na kufa. Kitendo cha kutovuna mazao haya ni hasara kwa Taifa na hatunufaiki na chochote kwa siku zijazo kwa kutovuna mazao hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwa kumkumbusha Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango, kuwa Mafia tuna chanzo cha mapato kitokanacho na watalii wanaoingia katika hifadhi ya bahari. Tunaomba chanzo hiki kikusanywe na TRA Mafia badala ya hifadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.