Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Saul Henry Amon

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rungwe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. SAUL H. AMON: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante nashukuru kwa kunipa nafasi hii kuchangia mpango wa bajeti ya mwaka 2019/2020. Kwanza kabisa naanza na pongezi kwa sababu nilisikiliza Mheshimiwa Dkt. Mpango alivyoisoma mwanzo hadi mwisho, alinikuna sana kwa ufupi, kabla ya yote, naunga mkono bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina mambo mawili matatu ya kuchangia kwa sababu ya muda naomba sijaona vizuri juu ya wafanyabiashara, kwanza tunaanza na hoteli. Watu wamelalamika, lakini watu wafanyabiashara wanatakiwa walipe hotel levy, wanatakiwa walipe sales levy, wanatakiwa kukusanya VAT, TARA imo ndani ya hoteli, kwa kweli ni mzigo mkubwa sana. Naomba hilo liangaliwe ni namna gani wafanyabiashara hawa wanaweza kutengenezewa utaratibu wa kodi. Nilidhani mimi kama mimi kwamba, kama mtu anayekusanya VAT, hao watu wa Manispaa na Halmashauri za Miji wasikusanye hiyo hotel levy kwa sababu inamkandamiza sana mfanyabiashara, hilo naomba liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili sheria hapa zimetungwa na zinatungwa vizuri sana, tatizo ni wale wanaokwenda kutengeneza hizo kanuni za kutumia hizo sheria. Nitatoa tu mfano mdogo, Serikali haiwajibiki kumkinga mfanyabiashara au kumuwekea kifua kwamba, nitoe mfano mfanyabiashara ameingia mkataba na kampuni fulani huko nje alete mzigo hapa Tanzania, lakini kuna baadhi ya kanuni zinamkingia kifua huyo mfanyabiashara alete hizo biashara peke yake hapa Tanzania; hiyo haikubaliki na haiwezi kuleta ushindani ulio sawasawa, kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haitaleta ushindani ulio sawasawa kwa sababu huyu atakuwa anapanga yeye mwenyewe bei, yeye mwenyewe ataweka bei ya juu na Serikali itakosa mapato kwa sababu mzigo atakuwa anaingiza yeye peke yake. Nitatoa mfano, hapo nyuma kulikuwa na uingizaji wa maziwa ya watoto yanaitwa Info Care, lakini ukienda kwenye maduka yote South Africa inauza shilingi 3,000 ambapo mtu angeweza kuleta angeuza 7,000/ 8,000 lakini ka sababu Serikali imemkingia mtu kifua maziwa hayohayo yanauzwa elfu 20 hapa Tanzania kwa sababu, anaruhusiwa kuleta mtu mmoja. Biashara ya ushindani haiwezi kwenda na Serikali haiwezi kupata mapato kwa sababu anayeruhusiwa kuingiza ni mtu mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na ninaomba hilo lizingatiwe waliangalie watunga kanuni. Mtu akiingia mkataba na kampuni, kati ya kampuni na kampuni, mfanyabiashara na mfanyabiashara, Serikali inaingiaje? Acha kila mtu alete hizo bidhaa hapa na kila mtu aweze kuuza kadiri anavyotaka, mlaji ndio aamue na soko liamuliwe na bei itakayouzwa na mlaji. Hilo nimeliona na muliangalie vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nilikuwa nazungumza kwenye upande wa kilimo kuna kilimo ambacho kimeingia na kimepamba moto na kilimo chenye tija sana cha maparachichi, lakini bei ya miche ni kubwa mno. Naomba Mheshimiwa utusaidie kupitia Waziri wa kilimo watutengenezee miche mingi, bei ya 3,000 Wananchi wengi wanashindwa kukianza hicho kilimo, lakini muitikio ni mkubwa kwa Tanzania nzima, naomba huo msaada mtusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yangu yalikuwa ni hayo matatu. Na vilevile l nne ni kwamba, kuna hili suala la ukaguzi wa mizigo wa TBS huko nje ya nchi, najiuliza hivi ukaguzi unavyofanywa nje ya nchi ni kwa faida ya nani kwa sababu, tunalipa nje, kwa nini tusilete mizigo hapa, tulipie certificate tuwenazo hapa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano unapokwenda kununua sukari unajua kiwanda ni… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)