Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Awali ya yote nishukuru Wizara kwa kurudisha Ofisi ya Ardhi Kanda ya Kati ambayo ilikuwa Mkoa wa Morogoro; na ilikuwa haiingii akilini sana watu wanatembea kilomita zaidi ya 700 kutoka Mlimba, Malinyi, Ulanga, kuja Dodoma kufuata huduma za ardhi. Kwa kweli kwa hilo wana wa Morogoro wameshukuru kwamba sasa tunakwenda kupata zile huduma katika Kanda yetu ya Kati.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikimfuatilia sana Mheshimiwa Waziri kwa jinsi anavyoeleza, anajipambanua kwamba masuala ya migogoro ya ardhi o kwenye fingertips zake, na hata wakati mwingine Wabunge wanapouliza maswali anadiliki hata kusahihisha.

Mheshimiwa Spika, yako mambo mengi ya kujiuliza, kama kweli Waziri ana master mambo haya ya migogoro ya ardhi, kwa nini migogoro inaendelea? Inashangaza kuona kwamba Waziri anazunguka, kila mahali yupo; na mimi ninavyoelewa, Waziri ni taasisi. Waziri unapobeba mafaili unakwenda kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za ardhi na camera pamoja na mavumbi yote wakati una watu pale ambao wangeweza wakaifanya hiyo kazi tunaona bado kuna shida mahala fulani. Haiwezekani Waziri inabeba hati mfukoni unakwedna kugawa kwa watu sijui mia ngapi ambao hawajapata ardhi kwa zaidi ya miaka 15.

Mheshimiwa Spika, hiyo kazi, ilipaswa, a-delegate kwa watu. Kwa maana kama Waziri unahangaika kufanya haya yote kushughulika na migogoro, lazima watu walioko chini yako wafanye kazi ambayo unaifanya wewe!

Mheshimiwa Spika, lingine, tumemsikia Waziri anasema, ameanzisha mpaka kipindi cha kusema a…

SPIKA: Kwa kweli Devotha mnapolalamika Wavunge kwa miaka kadhaa watu wangu hawajapata hati, Waziri anatoka ofisi anakuja kuhakikisha watu wenu wanapata na kuwapa yeye mwenyewe. Hilo nalo ni kosa pia? Labda utuwekee vizuri (Makofi)

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, ninachokizungumza, kama Waziri ameanzisha mpaka kipindi anasema cha kupambanua, watu watoe hoja zao na kero zao. Hivi migogoro ya ardhi ilivyo mingi kwa watu zaidi ya milioni 50, kila mmoja akiamua kupambanuka kwa Waziri kueleza atatue migogoro yote ya ardhi peke yake ataweza? Ninachokiamini Waziri ni taasisi, wasaidizi ni lazima katika Mikoa, kwenye Ofisi za Ardhi wafanye kazi hiyo hiyo, ndiyo ninachokimaanisha, kwamba sasa kama Waziri atakwenda kutoa hati na kuna DC, kuna Afisa Ardhi, hizo kazi zingine alipaswa a-delegate watu hawa…

SPIKA: Mtoa taarifa tafadhali nakupa ruhusa, ni Mheshimiwa Getere.

TAARIFA

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Devota kwamba amekiri kwamba migogoro ya ardhi ni mingi sana katika nchi hii na Waziri kutokana na migogoro hiyo ndiyo inampa jukumu la kwenda kuangalia nini kifanyike ili migogoro ipungue. Sasa kisa cha kumwambia, kwa hiyo maana yake kwa lugha nyingine ni kwamba Waziri aendelee kukaa ndani wakati migogoro inaharibu, anatoa maagizo kila mahali na pale inapoona inabidi kwenda, anaenda kuiona ili amalize mgogoro. Ahsante.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Devota unapokea taarifa hiyo dakika zako ni chache nazilinda hapa.

MHE. DEVOTA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kulinda ninachomaanisha mimi kama Waziri ndiye anayefanya kazi basi kazi hiyo ionekane pia kwa wasaidizi wake, wafanye kazi kwa namna hiyo ndiyo ninachomaanisha.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo ninalizungumzia ni kuhusu bomoa bomoa. Nilitegemea Waziri angeeleza jambo kuhusu bomoa bomoa ya Dar es Slam Ubungo, Kibamba, nyumba zaidi ya 1,300. Watu hawa ambao walibomolewa nyumba zao wakiwa na hati mikononi, wengine wakiwa na title mikononi, mpaka watu hawa wavunjiwe tulitaka kujua Maafisa hawa waliotoa.

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Devota, nalinda muda wako usiwe na wasiwasi, Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara.

TAARIFA

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) Mheshimiwa Spika, nimpe taarifa Mheshimiwa Devota Minja kwamba suala la bomoa bomoa la Dar es Salam na hasa anayozungumza Kibamba kwenye maeneo ya road reserve ya barabara ile. Moja ni kwamba watu walilipwa fedha wengine wakaondoka, wengine hawakuondoka, waliobaki wakawauzia wageni ambao hawakuwa na taarifa kwamba eneo limelipwa fidia. Walipoambiwa kwamba eneo litabomolewa wakaenda Mahakamani, wakaenda wakashindwa kesi na Serikali ina hukumu hapa. Katika hali ya kawaida Serikali ilitekeleza maamuzi ya Mahakama ya Juu ya Ardhi. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Devota, maliza dakika zako, kwa hiyo waliingizwa mkenge.

MHE. DEVOTA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, ninachokisema hapa ni kwamba, kama watu walilipwa fidia na wakauza na watu wengine wakarasimishwa, lakini watu hawa hawa kuna myumba zingine zimejengwa pale na tunaamini kabisa kuna Ofisi za Mipango Miji wametoa wapi ramani, zimepitishwa na nani na ni kwa nini watu hao hawakuwajibishwa. Kuna watu wamepelekewa umeme, kuna watu wamepelekewa maji, kwa nini watu hawa hawakuwajibishwa? Kujenga nyumba si rahisi watu wanajenga nyumba kwenye ujana wao mpaka wanazeeka hawajamaliza...

SPIKA: Mheshimiwa Devota utakuwa unabishana na Mahakama sasa, maana yake tumeambiwa Mahakama ishahukumu hilo, utaanzisha tu kesi ambayo yaani, kwa kuwa Mahakama ilishafanya basi kanuni zetu zinasema sisi hebu hatuwezi ku-question, endelea Mheshimiwa Devota.

MHE. DEVOTA M. MINJA: Mheshimiwa Spika, hoja yangu ni kwamba suala la ubomoaji linahitaji busara pia, maendeleo yanahitajika, lakini lazima pia tuangalie kama kweli Serikali inajipambanua kwamba ni Serikali ya wanyonge, ilipaswa kuliona hilo na kuwasaidia hawa watu kuliko hasara ambayo watu hawa wameipata.

Mheshimiwa Spika, lingine baya zaidi ni pale kunapokuwa na kauli za kibaguzi kwamba watu ambao wako Mwanza wamepiga kura kwa CCM, hao hawatabomolewa, lakini walioko maeneo mengine wanabomolewa…

SPIKA: Muda umeisha, dakika zako zimeisha, Mheshimiwa Devota.