Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ningependa kuunga mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Ningependa kupata majibu ya Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya usambazaji umeme ndani ya Jimbo la Mlimba, pia ulipwaji wa fidia kwa wananchi kama nitakavyoainisha hapo chini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa low cost ambao ulitekelezwa Jimbo la Mlimba tangu Kata ya Mchombe hadi Idete. Mradi huo pamoja na viongozi kadhaa kutembelea na kuzisikia na kuziona changamoto na kuahidi kuzitatua tangu mwaka 2017/2018; zilizosababishwa na mkandarasi; za kupitisha nguzo kwa rushwa na kukwepesha mradi eneo la makazi na kupitisha porini. Eng. Msofe tulipoongozana naye aliwasikia wananchi Kata zote za Idete, Namwawala, Mbingu, Igima na Mchombe.

Mheshimiwa Spika, Pia Waziri Mheshimiwa Dkt. Kalemani, Mbunge alifanya ziara na kusikia kilio hicho na kuahidi wananchi na kumuagiza meneja ahakikishe anapeleka umeme kwenye mradi huo na Wizara itapeleka vifaa vya mradi huo ili wananchi wapatiwe umeme. Lakini hadi leo hakuna mabadiliko yoyote kwenye mradi huo na kufanya maagizo yote na ahadi ni hewa. Je, ni lini sasa Wizara itatatua matatizo kwenye mradi huo?

Mheshimiwa Spika, kuhusu ufikishaji wa umeme kwenye maeneo ya huduma za umma kama shule, zahanati na masoko. Niliuliza swali Bungeni na kuwasiliana na Mheshimiwa Waziri kuhusu mradi unaoendelea sasa, ambapo unapita jirani na Sekondari Kata ya Kamwene lakini mkandarasi hana bajeti ya kupitisha umeme na Waziri aliagiza umeme upelekwe huko na Sekondari ya Matundu Hill, Idete; lakini hadi leo hakuna utekekelezaji. Je, ni lini agizo hili la Waziri litatekelezwa?

Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia kwa wananchi wa Kata ya Utengule, Jimbo la Mlimba ambao walikubali kupisha mradi wa umeme mkubwa kutoka Kihansi kwenda Wilaya ya Malinyi. Wananchi wa Kijiji cha Mpanga walifanyiwa tathmini tangu mwaka 2014; pamoja na ahadi nyingi lakini hadi leo hwajalipwa.

Mheshimiwa Spika, nimeambatisha document za ufuatiliaji.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni lini kituo cha kupoza umeme kitajengwa Ifakara ili wananchi wa Kata ya Mofu ndani ya Jimbo la Mlimba watapelekewa umeme kama Mheshimiwa Waziri Dkt. Kalemani ulivyoahidi? Kwamba Kata hiyo hiyo watapelekewa umeme baada ya kituo hicho kujengwa?

Mheshimiwa Spika, nasisitiza, kwamba Mheshimiwa Waziri awe na ufutiliaji wa karibu wa wakandarasi kwani miradi mingi inafanywa chini ya kiwango. Kwa mfano, mradi wa Mchombe - Idete, mradi wa Kihansi – Malinyi na kadhalika. Pia naomba kituo cha Mlimba kiongezewe gari la kazi kulingana na miundombinu yetu ambayo ni mibovu, hivyo meneja na mafundi hushindwa kufikia maeneo.