Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Alfredina Apolinary Kahigi

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Medard Kalemani, Naibu wake, Mheshimiwa Subira Mgallu pamoja na watendaji wote wa Wizara. Mungu awatie nguvu kwa kazi yao hii ngumu, tuonaona wanavyochapa kazi. Maoni yangu ni kwamba katika Wilaya yangu ya Bukoba Vijijini bado kuna kata nyingi ambazo umeme haujafika, ni nyumba chache zimepata umeme, REA I, II ilikuwa unarukaruka nyumba nyingi, nikiwa na maana vitongoji na vijiji.

Mheshimiwa Spika, nashauri Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu tusaidiane ili walau wapate nao mgao huo. Kuna wenye viduka vyao wanahitaji vitu vingine kuweka katika friji lakini wanashindwa, wanatumia jenereta. Mafundi wa magari kuchomelea vyuma umeme ni shida wasaidie wananchi ili kazi zao ziende vizuri.

Mheshimiwa Spika, lingine, katika vijiji hivyo kuna vitongoji ambako kuna zahanati; katika zahanati hizo kuna dawa zinazopaswa kuhifadhiwa katika friji; umeme hawana na hivyo dawa zinaharibika. Niwaombe hilo liangaliwe kwa jicho la huruma, siwezi kutaja ni vijiji vingapi, ni vingi havina umeme.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu najua ninyi ni wasikivu san sana. Maoni yangu msiyatupe katika dustbin tufikirie tupatiwe walau sehemu kubwa, wanufaike na umeme.

Mheshimiwa Spika, mwisho nawatia moyo Mungu awabariki sana, lakini tukumbuke sana Bukoba Vijijini umeme ni shida. Ahsante.