Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Julius Kalanga Laizer

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Monduli

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. JULIUS K. LAIZER: Mheshimiwa Spika, kwanza niwapongeze Wizara hasa Waziri, Naibu Waziri na viongozi wote kwa juhudi kubwa wanazofanya kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata umeme wa REA na wa uhakika.

Mheshimiwa Spika, la pili; namshukuru Mheshimiwa Waziri yeye binafsi kwa jitihada ya kupeleka umeme katika chanzo cha maji-Makuyuni. Wananchi wa Monduli wanamshukuru sana na wanamwombea kwa Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru pia kwamba katika mpango wa REA III, phase III Julai mwaka huu Monduli katika vijiji takribani 28 tumewekwa katika mpango, lakini kwa bahati mbaya vijiji viwili muhimu vimeachwa. Ombi letu, vijiji hivyo viongezwe yaani Kijiji cha Lashaine, Kata ya Lashaine na Kijiji cha Migombani, Kata ya Majengo. Hata hivyo, katika REA Awamu iliyopita line kubwa imepita katika vijiji, lakini wananchi katika vitongoji vingi hawajaunganishwa, nini mkakati wa kusaidia wananchi hao kupata umeme?

Mheshimiwa Spika, ushauri wa jumla; Serikali iwajengee uwezo TANESCO ikiwemo rasilimali watu ili waweze kutekeleza miradi ya REA badala ya kuwatumia Wakandarasi ambao wamekuwa wanachelewesha kazi. Hii itapunguza gharama na miradi itaisha kwa wakati.