Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia hoja hii hasa katika suala la miradi ya umeme vijijini REA III hasa kwa Mkoa wa Iringa. Hadi sasa jumla ya wateja 3,541tu kati ya wateja 13,556 ndio wameshaunganishiwa umeme katika vijiji 67 kati ya vijiji 179. Hii spidi ni ndogo na vijiji vingi havijapata umeme huu hasa Jimbo la Kalenga, Kata ya Luhota, Vijiji vya Tagamenda, Wangama, Kitayawa na Kata ya Mgama na Mseke kuna baadhi ya vijiji havina umeme.

Mheshimiwa Spika, nashauri hata vijiji vilivyowekewa umeme ni nyumba chache sana zenye umeme na hata maeneo ya shule, zahanati nazo bado hazijapata umeme. Hivyo Serikali iweze kuweka umeme katika Jimbo na Kata zake zote pamoja na vijiji vilivyopo katika jimbo hilo. Niliuliza swali la msingi na majibu yalikuwa kwamba hii REA III itamaliza matatizo katika jimbo hilo na mkoa kwa ujumla, naomba bajeti hii iziangatie hilo.