Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana. Naomba na mimi nichangie kwenye Wizara hii ya Nishati na Madini. Nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwa kazi nzuri anayofanya; Mungu akubariki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niseme, kama taifa tunahitaji umeme mwingi, na kama ingewezekana leo tukawa na uwezo wa kuzalisha megawatt 10,000 ingelipendeza zaidi. Mimi nimpongeze sana Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni muasisi wa taifa letu. Mwalimu Nyerere alikuwa na maoni ya kama Taifa la Tanzania tuwe na utoshelevu wa Nishati ya umeme na Mwalimu Nyerere wakati ule alikuwa na maono ya Stiegler’s Gorge. Sasa bahati mbaya sana wakati ule kama Taifa tulikuwa tunahitaji megawatt 100 na uwekezaji kwenye Stiegler’s Gorge usingewezekana kwa sababu gharama ilikuwa kubwa. Lakini wakati ambao tunao ni wakati mwafaka wa kuwa na umeme unaotokana na Stiegler’s Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna watu wana hoja dfhaifu sana. Hivi wanataka watuambie kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa mjinga, kwamba hakuwa na maono sahihi? Mimi nikuambie, kama kuna mtu anapingana na maono ya Mwalimu Nyerere huyo mtu amelaaniwa. Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa principle, mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa maono, amekufa mzee wa watu hana chochote hana lolote kwa sababu alikuwa na uzalendo mkubwa na nchi hii. Leo nani anayeweza akasema mimi ni mzalendo kuliko Nyerere? Leo watu wanasema issue ya mazingira, mazingira kitu gani? Wananchi wa Tanzania wangapi wanatumia kuni na mkaa? Misitu mingapi inafyekwa kwa ajili ya mkaa na kuni? Tuambizane hapa kwa kuja na takwimu. Mimi huko ninakotoka kila mtu anatumia mkaa, kila mtu anatumia kuni, misitu inafyekwa kila leo. Leo sehemu ambayo inafyekwa kwa ajili ya kuwekeza ni sehemu ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, umeme wa maji ni umeme wa gharama ndogo. Unajua mimi kitu siwaelewi watu wa kule upinzani, hawaji na statistics, research. Leo tuambieni umeme wa gharama ndogo ni upi kwa research ni upi? Umeme wa gharama ndogo ni umeme wa maji; shilingi 36. Sasa ukiwasikiliza hivi hawa wako sawasawa kweli? (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini bahati nzuri unajua mimi nimetokea kule unajua kule ili mtu achangie mpaka ale ile kitu ya kwao Heche kule Tarime.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanasema waemacha gesi, wameacha gesi wapi? Kwa taarifa yako asilimia 50 ya umeme tunaoutumia unatokana na gesi. Hawasemi hilo, hawasemi kabisa. Leo nimepigiwa simu, kuna watu wana magari yanatumia gesi, hiyo hiyo gesi yanatumia, na kesho Mheshimiwa Waziri amesema wayalete hapa Bungeni Wabunge waone magari yanayotumia gesi yetu. Sasa labda hawajui master plan ya nishati yetu. Our master plan is power mix, energy mix. Labda tu niwaamabie kwa dondoo kidogo ili waelewe. Upepo kwa research iliyofanyika utazalisha megawatt 500, solar 500, maji megawatt 5,000. Sasa uache umeme wa maji 5,000 uende kwenye nini? Wewe tulia, huelewi! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uwekezaji wa umeme huu wa Stiegler’s Gorge ndio rahisi kulingana na mazingira ya kiuchumi tuliyonayo. Huwezi kujigamba kwenda kuwekeza kwenye umeme wa ghali ilhali tuna shida nyingine. Tuwekeze kwenye huu ambao ni very cheap lakini umeme mwingi halafu utashuka bei; unajua hofu ni 2020 inawatesa wale jamaa wa kule ng’ambo. Ikifika 2020 wataenda kusema nini? Sasa hivi REA kila kijiji watakuwa wamepata umeme au nasema uongo? Kila kijiji watakuwa wamepata umeme, kwa hiyo wanahaha, wenzenu wana shida kweli kweli, hawalali! Sasa wewe unafikiria mtu kama yule Mnyika, atarudi wapi? Au yule Sugu, anarudi wapi? He! (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nikwambie kinachowatesa ni hofu ya kutokurudi 2020; na kwa kazi ambayo anaifanya Rais Magufuli mimi nasema Rais Magufuli kamua twende. Nilikuwa nasoma kwenye kitabu cha Kambi ya Upinzani yaani ni kituko. Yaani kweli, taarifa gani hii? Uongo mtupu!

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nilikuwa najua Mnyika ni Padri kumbe anasema uongo. Hebu sikiliza hii, eti Mnyika anaema TANESCO ina madeni inashindwa kujiendesha sijui kitu gani. Hebu sikiliza, TANESCO enzi za nyuma ilikuwa inapewa kila mwaka bilioni 143 ruzuku ya Serikali, mwanaume Magufuli alipoingia akasema hakuna cha ruzuku mtajiendesha wenyewe; kwa kuwa ninyi ni Shirika la Serikali, lazima mzalishe faida. Mwaka 2017 TANESCO mapato ambayo imekusanya ziada 1.5 ziada! Na wanalipa kila wiki 9 billion TPDC, wewe unasema nini? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Chacha, ahsante sana muda wako umekwisha. Ahsante sana. Muda umeisha.

MHE. CHACHA M. RYOBA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. Mheshimiwa Kalemani songa mbele, ahsante sana. (Makofi)