Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati. Kwanza kabisa naiunga mkono kwa asilimia mia moja. Pamoja na kuunga mkono nataka nimpongeze Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Kamishna na watendaji wote wanafanya kazi nzuri sana. Zamani hali ya maisha vijijini tulikuwa tunatumia taa za kawaida vibatari, lakini sasa hivi karibu vijiji vingi Tanzania hapa wananchi wana umeme. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri achape kazi sisi tuko pamoja naye, afanye kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Mpwapwa karibu vijiji vyote vina umeme, Jimbo la Mpwapwa ni vijiji nane tu ambavyo havina umeme lakini zaidi ya vijiji 58 vina huduma ya umeme. Naomba tu kwamba ulivyoahidi pale Kijiji cha Igoji-I kwamba baada ya kusambaza umeme kwenye vijiji sasa wataanza kusambaza umeme kwenye vitongoji. Vitongoji ni vingi na kule ndipo wananchi wengi wanaishi. Kwa hiyo naomba huu mradi wa kusambaza umeme vitongojini nao vilevile uanze.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru Mheshimiwa Waziri Jimbo la Mpwapwa amefika vijiji vine; amefika Tambi kuzindua umeme, Mbori, amefika Igoji-I na kile kijiji kimoja cha Jimbo la Kibakwe. Kwa hiyo tumshukuru sana ni mara chache sana Waziri anafika anafanya ziara katika mwaka mmoja katika vijiji vinne. Kwa hiyo namshukuru sana

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ni kuhusu kukatika katika kwa umeme. Wilaya ya Mpwapwa line ambayo inasambaza umeme inapeleka umeme Mpwapwa, ni line ambayo inapeleka umeme vilevile Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Gairo, Wilaya ya Kongwa pamoja na Wilaya ya Mpwapwa. Hivi karibuni wameanzisha tena umeme line ile ile ya Mpwapwa, wamechukua Kijiji cha Mpwayungu pamoja na Mwitikila kule Wilaya ya Bahi. Kwa hiyo hii line imekuwa over loaded, sasa nashauri mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wilaya ya Mpwapwa tujengewe line mpya itakayoanza Zuzu, Kikombo Station, Kiegea na pale najua umeme ukifika Kiegea hata Kazania watapata umeme line hii ikitoka Kiegea iende Mbande na pale Mbande wanajenga substation na hii substation watajenga line moja, moja kwa moja kwenda mpaka Mpwapwa ambayo itajulikana kwa jina la Mpwapwa feeder badala hii line. Hii line kwanza nguzo zote zinapita kwenye madimbwi ya maji huku kwa hiyo ndiyo maana umeme unakatika katika kila wakati, lakini maeneo mtakayopitisha line mpya Mpwapwa hakuna madimbwi ya maji ni eneo kame kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo na nne kuhusu gharama za umeme;gharama ni kubwa. Nashukuru sana alitangaza kwamba gharama ya umeme ni shilingi 27,000 kuvuta umeme kwenye majumba. Sasa umeme kati ya TANESCO na REA basi ulingane ufanane, maana mwingine Sh.177,000 mwingine Sh.27,000, naomba sana gharama za umeme zipungue ili wananchi wengi waweze kuvuta umeme kwa sababu gharama zikiwa kubwa wananchi watashindwa kuvuta umeme kupeleka kwenye majumba yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuzungumza hayo naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri, ahsante.