Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Mbele yetu ni Wizara nyeti katika Taifa letu na hasa katika shughuli nzima za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni kama kufanya business. Na ili ku-operate business kubwa lazima uwe na investiment kubwa, kuwe na brain kubwa ambayo unaiweka katika business unayotaka kuifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muda mrefu sana nimekuwa Mbunge sasa wa miaka tisa, lakini katika Wizara hii imekuwa ni kutatua migogoro ya Loliondo na wafugaji, kutatua migogoro ya watu wa Ngorongoro na wafugaji, kutatua migogoro ya TANAPA na wananchi, mipaka ni tatizo. Imekuwa ni kutatua migogoro ya maeneo chepechepe, kwa mfano kule Kilombero, Ihefu na wananchi. Kwa hiyo, badala ya kufanya business tunajikuta kama Taifa tuko busy kutatua migogoro badala ya kusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani ni wakati muafaka kama Serikali tufike mahali tuseme enough is enough, tufanye biashara inayotokana na Wizara hii, kwa sababu, migogoro imekuwa mingi hatutoi suluhisho la kudumu katika masuala ya mipaka, kwenye maeneo oevu, kwenye maeneo ya hifadhi, hatujatoa suluhisho la kudumu. Hatuwezi kuendelea kama tunaendelea kukaa chini na kutatua migogoro badala ya kufanya business na kushindana kimataifa namna gani tuweze kufanya hii biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo napenda nizungumze kwa upana sana eneo moja. Kumekuwa na biashara ya viumbe hai, wanyama hai ambao wamekuwa wakisafirishwa. Biashara hii imekuwa ikifanywa toka wakati wa mkoloni na wakati wa mkoloni ni wazungu tu walikuwa wanasafirisha, mpaka mwaka 1974 ikabadilishwa wakawa wanafanya wazawa peke yao. Sasa kwa bahati mbaya sana hawa watu wamefanya biashara na wamefanya kwa mujibu wa sheria, lakini kama hotuba yetu ilivyosema ghafla wakati wa Mheshimiwa Maghembe biashara hii ilisitishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilisitishwa wakati watu hawa wameshafanya maandalizi, wamekamata wanyama wamewaweka kwenye holding grounds, wamekopa mikopo, wamefanya contact na wateja wao duniani kote, ikaja hii biashara ghafla ikasitishwa. Watu hawa hii biashara hawafanyi wanyama ambao wako kwenye National Parks, kwenye Game Reserves, wanafanya biashara ya huku porini ambako kuna nyani, kuna ngedere, kuna spiders, kuna konokono na nyoka na mijusi, vitu ambavyo havitumiki kwa biashara nyingine katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hawa watu baada ya Serikali kusitisha wameingia katika umasikini mkubwa sana, wengine mpaka juzi nimesikia wamekufa. Ningeomba Mheshimiwa Waziri hebu tutoe jibu kwa hawa watu ni kwa namna gani tutawalipa fidia, hawa ni Watanzania. Ukiangalia biashara hii ilikuwa inaongeza pato la Taifa, fedha yake inayotumika asilimia 100 Serikali haiingii hasara na tunapata fedha ya kigeni, hawa watu wamefanya kazi kubwa sana kulikuwa na wakamataji, kulikuwa na mahoteli, ikasitishwa na wengine mpaka walikufa, wale watu waliopelekwa Mahakamani mpaka leo walishinda kesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wameendelea kuwatesa, tumewa-cripple, ningeomba Serikali itoe jibu lake; wametoa malalamiko kwako Waziri, Waziri aliyepita, wametoa kwa Rais, naomba hawa watu Mheshimiw Waziri awaangalie kwa jicho la huruma. Muda mwingi tumezungumza watu wengine sana, hawa ni wafanyabiashara wadogo wadogo na ni Watanzania wazawa ambao walikuwa wanajitahidi kujitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kibaya zaidi Serikali huwa inatumia pesa nyingi kuangamiza ndege kama kwelea kwelea. Kwa mfano kuna wakati waliuwa ndege karibu milioni 70, sasa unapoua wale ndege dawa zile wanaposhusha kuwaua wale ndege, dawa zile zinaua na mijusi na hao nyoka ambao wale watu wangewasafirisha tukapata hela. Sasa haya ni mambo ambayo hebu tuangalie namna gani tunaweza tukafanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza hapo mwanzoni hii biashara ni business na namshukuru Waziri ni mfanyabiashara, lazima ana business mind. Wizara hii tukiichukulia kama Wizara nyingine bila kuwa na upeo wa kibiashara hatuwezi kusonga mbele, hatuwezi kuingia kwenye ushindani, lazima kuwe na fikra za kibiashara. Katika maeneo mengine Mheshimiwa Waziri amefanya vizuri, siwezi kumkandamiza katika kila eneo; alitoa kwa mfano ile Tanzania Unforgetable, nilitamani sana ingetumika hata wakati wa Timu yetu ya Taifa, Tanzania Unforgetable, kuliko ile tuliyotumia “Sasa hivi ni Zamu Yetu”, tukienda nchi sasa hivi ni zamu yetu haiwezi kutusaidia, ingetusaidia kutangaza utalii, lakini tungelitumia hilo neno ni neno zuri ambalo linaitangaza nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ambalo wamefanya vizuri ni kwenye masuala ya ujangili. Wizara imefanya vizuri, hatuwezi kuwalaumu, nimekuweko kwenye Wizara hii ujangili kweli umeporomoka, lazima tuwapongeze katika hilo; lakini ninachosema kwenye eneo hili la hawa watu ambao wana shida, tumewatesa kiasi cha kutosha naomba Waziri atakaporudi atoe tamko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la sheria zinazokinzana; kuna sheria nyingi zinakinzana, Sheria za Ardhi, Sheria za Mazingira, Sheria za Maliasili, zinakinzana maeneo mengi kiasi kwamba, hazitekelezeki, Sheria za Madini, kuna maeneo mengi ambayo hizi sheria zinakinzana kila eneo. Ningeomba hili suala limalizwe ili tuache kukaa muda wote tunagombana na kutatua migogoro, tuwe tunafanya biashara tunashindana na watu wengine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, success is attracted, you don’t pursue success, ni lazima tutengeneze mazingira ambayo yata-attract mafanikio katika nchi yetu, lakini hatuwezi kutengeneza mazingira kama tuna watu wa aina ileile. Ili tu-attract success katika nchi yetu lazima tuwe na watu ambao wanavutia hayo mafanikio. Ni sawa na mbegu ya mahindi, mbegu ya mahindi ukiiweka kwenye simenti haiwezi kuota mpaka uitengenezee mazingira uweke maji, uweke udongo mzuri, uweke mwanga na oxygen, hewa, maana ndio itaota. Sasa tukiwa na watu ambao hawafikiri kibiashara, tukiwa na watu ambao hawafikiri Kitaifa, we have to think globaly and act local, lazima tubadili namna ya kufikiri katika namna nzima ya kuiendeleza Wizara hii ya Maliasili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba Mheshimiwa Waziri, najua wamefanya kazi kwa sehemu ambayo wanaenda mbele, kwa mfano wamefungua Television ambayo inatangaza nchi yetu, tutakuwa hatufanyi vizuri kama tusiposema mambo haya, hayo ni mambo mazuri ambayo lazima tuyapongeze kwa sababu tunataka tu- attract watalii zaidi. Hata hivyo, bado tunahitaji urithi tulionao na resources tulizonazo, it is highly time kwamba, tuchague, ni kwa kiasi gani Ngorongoro inatusaidia na tuna faida nayo. Tuchukue maamuzi ambayo yatatufanya Ngorongoro itusaidie, ni kwa namna gani maeneo oevu kama Kilombero yanatusaidia kama Taifa? Tufike mahali tuamue tunataka watu wachunge ng’ombe au tuache maeneo oevu ambayo yanasaidia mpaka kule Selou? Ni wakati muafaka tuangalie mipaka tuliyoipanga katika nchi yetu, tutaendelea kuwa na migogoro mpaka lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kupata vitu ambavyo ni standard kama tuna fikra ambazo ni sub- standard. Kuna watu wako under average wanataka wapate mshahara ambao ni above average, haiwezekani. Kwa hiyo, tunashindana na Mataifa mengine kama Botswana, tunashindana na Mataifa mengine kama South Africa, hatuangalii ni brain kiasi gani wame-invest katika tasnia hizo, ili wapate return kubwa. Huwezi ku-invest brain ndogo ukategemea upate return kubwa in terms of money, in terms of mipango, mambo mengi hayo yana-involve mipango mizuri, tumezungumza sana kuhusiana na masuala ya migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mambo matatu ambayo nimeyazungumza Mheshimiwa Waziri ni suala la viumbe hai wanaosafirisha ambalo kwa kweli wamewa- cripple, jambo ambalo sio sawasawa, lakini bado suala la pili nimezungumza kuhusiana na sheria ambazo zinakinzana ziko nyingi na kanuni ambazo ziko kwenye uwezo wao. Afadhali sheria labda zitachukua muda, lakini kanuni nyingi ziko kwenye uwezo wao wanaweza wakazileta hapa tukazirekebisha kuondokana na migogoro ili tufanye business.

Kwa hiyo, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, Wizara hii ni Wizara ambayo inategemewa kuleta mapato mengi katika nchi yetu, tufike mahali waache legacy katika Wizara hii, imekuwa ni Wizara ya kufukuza watu wengi, ya kubadilisha watu wengi, hapo nyuma tumegombanagombana, lakini kwa namna moja au nyingine sasa hivi kuna mwanga unaonekana, kuna kazi inafanyika. Wanasema mara nyingi hatusifu, leo Mheshimiwa Dkt. Kigwangala nisifu kidogo kuna sehemu ya kazi inafanyika, mambo madogo madogo yarekebishwe. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)