Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe wa kunipa nafasi hii ya kuchangia katika hotuba hii. Pili, napenda kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Waziri wa Kilimo pamoja na watendaji wake wote kwa kutayarisha na kuwasilisha hotuba hii kwa ufasaha mkubwa.

Mheshimiwa Spika, katika kutoa mchango wangu katika hotuba hii, napenda kuchangia kwenye maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Kilimo; naipongeza Serikali kupitia Wizara hii kwa kuweka utaratibu mzuri wa kutoa mafunzo ya kilimo kwa vijana wetu nchini. Hili jambo ni jema ambalo litatupelekea kulima kwa mtindo wa kisasa badala ya ule wa kufanya kazi kwa mazoea.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa Wizara ni kwamba, iweze kuwatumia wataalam wanaohitimu kwenye vyuo vyetu ili walete mafanikio. Wataalam hasa Mabwana/ Mabibi Shamba wawezeshwe ili waende vijijini badala ya kukaa mijini/maofisini. Wakulima wetu wa vijijini hasa wale wa kipato cha chini wanahitaji maelekezo ya kitaalam sana ili kufanikisha kazi zao.

Mheshimiwa Spika, pili, pembejeo za kilimo, Serikali yetu inajitahidi sana kutafuta miundombinu ya pembejeo. Kilimo ni uti wa mgongo hasa katika nchi yetu ambayo inaelekea kwenye siasa ya uchumi wa viwanda, bila ya kilimo hakuna viwanda, hivyo ni vyema Serikali ikawawezesha wakulima kwa kuwapatia pembejeo hizo.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu katika suala la pembejeo kwa Serikali kuweka bei wezefu ambazo wakulima wetu wa chini wataweza kununua/watamudu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.