Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Nami pia naungana na Waheshimiwa Wabunge kumpongeza Mheshimiwa Spika pamoja na Sekretarieti ya Bunge ikiongozwa na Katibu wa Bunge kufanikisha utumiaji wa e-Parliament ndani ya Bunge letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nikiwa kama Kamishna wa Bunge pamoja na wewe na wengine kwa muda mrefu sana tumekuwa tunashauri namna gani ya kuweza kuhakikisha kwamba Bunge letu linakuwa la kisasa, linaendeshwa kwa e-Parliament kama Mabunge mengine. Ukiangalia almost Mabunge yote ya nchi za Afrika ni Bunge letu pekee lilikuwa limebaki bado tunatumia karatasi na hivyo kuwa na malundo ya makarasi kwenye madawati yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa hatua tuliyofikia tunashukuru sana na tunamshukuru pia Katibu wa Bunge maana alipewa order kabisa. Mheshimiwa Spika alifika mahali akatoa order kwamba ifikapo Bunge hili la mwezi Novemba kama Wabunge watakuwa hawajapata tablets kwa kweli hapataeleweka na aliweza kutumia muda huo mfupi kuhakikisha kwamba anafanikisha azma hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naungana na Wabunge kuwashukuru sana Sekretarieti na hasa watumishi wa Idara ya IT kwa kazi kubwa waliyoifanya kuwezesha Wabunge kutumia teknolojia hii mpya. Wametumia muda wao mwingi ndani na nje ya Bunge kutuelimisha ili kila Mbunge aweze kutumia kifaa hiki na kuhakikisha kwamba tunafuatilia shughuli za Bunge kwa ukamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi tablets hizi bado zinatumika ndani ya Bunge peke yake lakini kwa maelekezo ya Mheshimiwa Spika pia kifaa hiki kiweze kutumika vizuri Wabunge wote ku-access information kwenye tablet zao nje ya Bunge na hata majimboni mwetu. Kwa hiyo, ni matumaini ya Wabunge kwamba ifikapo mwakani kila Mbunge ataweza kutumia kifaa hiki akiwa ndani ya Bunge, nje ya Bunge na jimboni kwake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Naunga hoja mkono, ahsante. (Makofi)