Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

Hon. George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kwa Uamuzi wake wa Kulifanya Bunge Kutekeleza kwa Vitendo Dhana na Bunge Mtandao (e-Parliament)

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuunga mkono Azimio hili la Kumpongeza Mheshimiwa Job Ndugai, Mheshimiwa Spika wa Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naunga mkono kwa asilimia mia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uamuzi huu wa busara alioamua Mheshimiwa Spika kwa kweli utaleta faida kubwa sana katika Bunge letu. Kwanza kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Bunge kwa ajili ya kununua makaratasi, karatasi zilikuwa zinalundikana kwenye meza hasa wakati wa bajeti. Karatasi, vitabu vya bajeti vilikuwa ni vingi kweli kweli. Kwa hiyo, nampongeza sana kwa kutekeleza Azimio hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa na ndiyo tumejadili Muswada wa Sheria wa Serikali Mtandao. Kwa hiyo, Spika aametekeleza yale ambayo tumekubaliana katika Kamati yetu kwamba Serikali sasa iingie katika Serikali Mtandao. Hii vilevile itasaidia ukataji wa magogo kwani sasa hivi ni mkubwa sana na kusababisha uharibifu wa mazingira kuwa mkubwa sana katika nchi yetu. Kwa hiyo, Serikali Mtandao na Bunge Mtandao itapunguza makaratasi na ukataji wa miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la tatu ni utunzaji wa nyaraka za Bunge. Nyaraka za Bunge hivi sasa zinatunzwa kwenye makabati. Kwa uamuzi wa Mheshimiwa Spika wa kuleta Bunge Mtandao utasaidia kumbukumbu au nyaraka za Serikali ziweze kutunzwa kwenye computer na vitu vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na naendelea kumpongeza Mheshimiwa Job Ndugai, Spika wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ahsante, naunga mkono. (Makofi)