Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuunga mkono hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ningependa kupata majibu ya Serikali kuhusu mahusiano ya ujirani mwema kati ya Kata ya Mngeta – Kijiji cha Ikule na Kikosi cha Chita JKT. Mimi Mbunge bado napata malalamiko toka kwa wananchi ambao walikuwa wanafanya shughuli za kilimo maeneo ambayo walikuwa wanaamini kuwa ni maeneo yao tangu enzi za mababu zao na ndiyo maana kuna makaburi na mazao ya kudumu ambapo Chita JKT inasema ni maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa wapo wazee wanasema Jeshi halijawahi na hakuna kumbukumbu zozote za mihutasari ya kijiji ya kukubali ugawaji wa ardhi toka kijijini hapo, lakini pamoja na wananchi hao kunyang’anywa maeneo ya mashamba yao, bado walikuwa tayari kukaa pamoja na kufanya mazungumzo ili kupata namna bora ya wakazi hao kupata mashamba ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa nilipoongea na Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Mwinyi aliahidi kushirikiana na wananchi kwa kupeleka vifaa vya kilimo cha kisasa Jeshini Chita na kufanya uzalishaji mkubwa na wananchi watashirikishwa kwa kupewa mashamba na kupata ujuzi wa kilimo bora ili wazalishe kwa wingi na kuondoa umaskini wa kipato kwa wananchi hao, kuwa wakulima wa nje (out growers). Tangu tuongee na mkakati huo ni miaka miwili sasa imepita, je, ni lini mpango huo utatekelezwa? Ahsante.