Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Susan Limbweni Kiwanga

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Mlimba

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze mchango wangu kwa kuunga mkono maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na nishauri Serikali ipitie hotuba hiyo kwa umakini, kwa umuhimu na kuchukua yale ambayo yatasadia Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni miaka mingi sasa Serikali imekaa kimya na haitoi suluhisho la ubinafsishaji viwanda nchini hasa Mkoani Morogoro. Mfano, Kiwanda cha Mazulia Kilosa, Kiwanda cha Spare Parts Mang’ula, Kiwanda cha Moprocco na viwanda vingi ambavyo vilipewa wawekezaji na kuviondolea mashine na kubadilisha matumizi ya viwanda hivyo. Hii inaondoa ajira kwa Watanzania, inakosesha soko la mazao ambayo yangetumika viwandani.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, napenda kupata majibu ya Serikali, ni viwanda vingapi vilivyobinafsishwa na kushindwa kuviendeleza/kubadilishiwa matumizi na hatua zilizochukuliwa Mkoani Morogoro?

Mheshimiwa Naibu Spika, biashara nchini Tanzania imekuwa ni maumivu makubwa kwa wafanyabiashara ndogo na kubwa. Mtu akitaka kuanzisha biashara anatakiwa kulipa kwanza kodi inayokadiriwa kwa mtaji alionao. Hata kama biashara imepata hasara au haikupata faida, lazima kodi aliyokadiriwa ilipwe. Je, kwa nini kodi isilipwe kutokana na faida?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kuna vyuo vya biashara (CBE) na kwa kuwa kuna wahitimu wanaohitimu: Je, Serikali haina haja ya kuwaunganisha wahitimu hao na wafanyabiashara wakubwa nchini ili nao wawe wafanyabiashara na kuliingizia Taifa kipato? Je, ni lini Wizara itawafikia wanyabiashara wakubwa na wadogo ngazi za wilaya na mikoa ili kupata changamoto zao na namna ya kuzitatua?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri Wizara ichukue hatua ya kukaa na Wizara ya Fedha ione namna bora ya utozaji kodi mbalimbali ili kukuza biashara nchini na kuepusha ufungaji wa biashara nyingi hasa za watu wa kati. Ahsante.