Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

Hon. Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Kwa sababu dakika ni tano nianze kwa kusema, suala la korosho tunamuomba Mheshimiwa Waziri alichukulie serious. Kama ambavyo Kambi ya Upinzani imeshauri wale wote ambao wamehusika, tumeona manyanyaso makubwa waliyoyapata watu wanaoitwa kangomba ambao walikuwa tayari kuwasaidia wakulima wetu lakini kumbe Serikali hii iko tayari kumkumbatia kangomba wa Kenya kuliko kangomba wa Tanzania. Kwa hiyo, naomba wale wote ambao wanahusika wawajibike, Waziri wa Sheria, Fedha na Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naangalia kitabu cha Mheshimiwa Waziri, nimeangalia kwenye suala la makusanyo ya Mafungu 44 na 60 na nimeangalia miradi ya maendeleo. Kwenye makusanyo mwaka 2018/2019 mlikuwa mmeweka makadirio ya shilingi milioni 20 point lakini 2019/ 2020 kwa maana ya mwaka huu ambao mnauanza mmeweka makadirio ya shilingi milioni tano. Sasa sielewi Wizara ambayo ndiyo kauli mbiu ya nchi, Serikali ya Viwanda, mmetoka kukusanya shilingi milioni 20 mmepanga kukusanya shilingi milioni tano. Nitaomba maelezo Mheshimiwa Waziri kwamba sasa mmeshaacha kufanya shughuli za kutengeneza miundombinu ya biashara na uwekezaji? Kwa nini makusanyo mmeshuka kwa kiasi hiki? Mnataka kupewa fedha nyingi lakini nyie hamko tayari kukusanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kwenye miradi ya maendeleo, fedha za ndani zilikuwa shilingi bilioni 100 kwa mwaka wa fedha huu tunaoumaliza. Hata hivyo, kwenye Fungu 44 kati ya shilingi bilioni 90 mmepelekewa shilingi bilioni 6.47 sawa na asilimia 6.5 kutoka Serikalini. Kwenye Fungu 60 kati ya shilingi bilioni 7 ambazo militakiwa mpewe Hazina mpaka leo haijatoa hata shilingi, hiyo ndiyo Serikali ya Viwanda mnayoihubiri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wakati unaweza ukasema hii Wizara haipo labda kwa matendo yake, hakuna mchango wowote kwenye nchi hii kwenye Wizara hii unaoonekana kwa macho. Mmekuwa watu wa kupiga kelele na propaganda, sijui ukiwa na brenda tatu una kiwanda, ukiwa na cherehani ni kiwanda, lakini kwenye uhalisia hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi natoka Mkoa wa Tanga ambao ulikuwa na viwanda vingi sana miaka ya 80 na 90. Naomba nikutajie baadhi ya viwanda ambavyo Mheshimiwa Waziri utakuja kuniambia hapa vilikuwa vya Serikali mmeshindwa kuvifufua, hamjabinafsisha, vimekufa. Mje mniambie hapa tangu Serikali ya Awamu ya Tano imengia katika viwanda hivi ni vingapi vinafanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwa na Kiwanda cha Mbolea (Tanzania Fertilizer Company), Kiwanda cha Nondo (Steel Rolling Mills), Kiwanda cha Blanketi, Kiwanda cha Amboni Plastiki, Karakana ya Railway, Sao Mill, Kiwanda cha Foma (detergent), Kiwanda cha Cheap board pale Mkumbara, Kiwanda cha Ngano, pembe imekufa na tulikuwa tunazalisha mpira Muheza. Naomba Mheshimiwa Waziri ukija hapa utuambie kwa Mkoa wetu wa Tanga ni viwanda vingapi vimefufuliwa tangu Awamu ya Tano imeingia madarakani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina suala la Wilaya yangu ya Muheza ninakotoka. Tulikuwa tunalia usiku na mchana na Mheshimiwa Mwijage ni shahidi nilikuwa namuambia kila siku napokutana naye, wakulima wakubwa wa machungwa na matunda nchi hii wanatoka Mkoa wa Tanga, labda na Iringa na mikoa mingine. Tunalima sana machungwa lakini sasa hivi wakulima wa Tanga na Muheza machungwa yamekuwa ni sehemu ya mbolea ya mashamba yao, machungwa hayana bei. Kipindi cha Awamu ya Nne chungwa lilikuwa linauzwa shilingi 100 mpaka shilingi 200 kwa mkulima anachuma anauza kwa bei hiyo, sasa hivi ni shilingi 15 mpaka shilingi 25, Serikali ya Viwanda hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakulima wanapata shida, wanafanya mengi. Nimeomba Kiwanda cha Machungwa Wilayani Muheza, tunapata shida, machungwa yanaoza na yanatupwa. Mheshimiwa Waziri uje uniambie hapa ni lini …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)