Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi ya kuchangia. Michezo, kama tujuavyo ni afya, ni furaha na yanaleta upendo. Duniani pote magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu la kupanda na kushuka, ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya moyo huepukika mapema kwa kufanya mazoezi, lakini hapa Tanzania Halmashauri nyingi hazina viwanja vya michezo na pia barabara zetu sio rafiki kwa watu kufanyia mazoezi, hakuna sehemu za watembea kwa miguu.

Je, kwa nini Serikali isikae chini ili Wizara hii na Wizara ya Miundombinu wakaweka mikakati iwe ni lazima wanapojenga barabara wahakikishe kuwepo na sehemu za wapita kwa miguu ili iwawezeshe wananchi kutembea?

Mheshimiwa Spika, vile vile ni vizuri katika sehemu za kazi pawepo na sehemu za kuogea ili wafanyakazi watembee kwenda kazini, wakifika ofisini wanaoga.

Mheshimiwa Spika, viwanja vyote vilivyotekwa na CCM katika kila Halmashauri virudishwe kwenye Halmashauri kwa kuwa vilikuwa ni vya Umma na wananchi wote wavitumie kwa ajili ya mazoezi.

Je, Serikali ina mpango gani kwa kukifufua kiwanja wa King Memorial kilichopo Mkoani Kilimanjaro katika Manispaa ya Moshi ili kianze kutumika? Ukizingatia kiwanja kile kina michezo zaidi ya saba lakini kipo tu pale wananchi wanapanda maharage wakati kiwanja kipo.

Mheshimiwa Spika, kulikuwepo na mchakato wa ku- design vazi la Taifa na fedha zilitumika kwa ajili ya vazi hilo, lakini hadi leo hatujapata mrejesho, zoezi hili lilifikia wapi? Je, ni lini mchakato wa vazi la Taifa utakamilika?

Mheshimiwa Spika, ni haki ya wananchi kupata habari lakini ni jambo la kusikitisha vyombo vya habari havipo huru na vimebanwa sana. Local channel za television tulielezwa zilitakiwa ziwe bure, lakini cha kusikitisha ni chombo kimoja tu cha TBC ndicho kinachotoa matangazo tena kwa upendeleo, hawatoi habari zote. Mfano, hata hotuba za Upinzani Bungeni hazijawahi kutangazwa na TBC.

Mheshimiwa Spika, magazeti hayana uhuru. Yakiandika ukweli huwa yanapewa adhabu ya kufungiwa. Je, huu ndiyo uhuru wa habari mnaoutangaza?