Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu za dhati kwako kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Pili, nipende kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na watendaji wake kwa kutayarisha na kuiwasilisha kwa ufasaha na kwa utaalam.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, michezo; napenda kuipongeza Serikali yetu kwa hatua inayochukua katika kuendeleza michezo. Michezo ni miongoni mwa mambo ambayo yanaonesha utambulisho wa nchi. Naipongeza Serikali kwa kuilinda na kuiwezesha timu yetu ya Taifa mpaka kufika katika hatua ya AFCON.

Mheshimiwa Spika, michezo ni hasara, Serikali inabidi iongeze juhudi ya kuisaidia timu yetu bila ya kujali hasara, bila ya kuisaidia hatuwezi kufika hatua ambapo tunaikusudia. Pia naishauri Wizara ichukue hadhari na iwe makini katika uchaguzi/uteuzi wa wachezaji na viongozi wa kuendeleza na kuendesha timu hiyo. Uchaguzi wa sasa hauridhishi hata kidogo kwa kuwa timu hii ni ya Taifa la Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ni vyema uchaguzi wa wachezaji uzingatie pande zote za Muungano.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.