Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, naomba kumpongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, taasisi zote zilizoko katika Wizara na watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, sekta ya michezo na burudani, iwapo itasimamiwa vizuri kwa kutenga bajeti ya kutosha itasaidia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa lakini pia michezo inaitangaza nchi kiutalii duniani.

Mheshiimiwa Spika, kwa mfano, michezo kama mpira wa miguu, riadha, wasanii wa muziki, wasanii wa vichekesho (stand up comedy), ngoma za asili na wasanii wa maigizo (sinema); hawa wote ni chanzo kikubwa cha mapato yao wenyewe na hata Serikali inaweza kupata kodi yake kwa kiwango kikubwa iwapo kutakuwa na uwekezaji wa kisasa kwa sekta hii. Naiomba Serikali iwekeze kwa kiwango cha kutosha katika Sekta ya Michezo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja asilimia mia moja.