Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia hoja hii katika vipengele vifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sanaa, michezo na utamaduni kama kichocheo cha fursa za kiuchumi na umoja na upendo kwa Taifa letu. Takwimu za ukuaji wa kiuchumi katika nchi yetu zinaonesha kwamba sekta hii inachangia zaidi ya asilimia kumi na moja ya pato la Taifa. Hii inaashiria kuwa tukiwekeza zaidi tunaweza kukuza na kuongeza zaidi pato la Taifa letu. Hivyo nashauri Wizara ya Fedha iongeze ukomo wa bajeti kwa Wizara hii ili iwekeze zaidi kwa sekta za sanaa, utamaduni na michezo, kwani bajeti katika Wizara hii ni ndogo sana. Tuwekeze kwenye vyuo vya michezo pia TASUBA na masuala ya utamaduni.

Mheshimiwa Spika, uhuru na haki ya kupata habari nchini; Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia na kusaini azimio la kimataifa la uwazi katika uendeshaji wa Serikali. Kupata habari wananchi ndio utawala bora. Imekuwa ni kawaida sasa wananchi hawaoni Bunge live kwa kuwa wanataka kuona wawakilishi wao wanapeleka hoja zao kwa Serikali. Hivi ni kinyume kabisa na haki ya kupata habari na masharti yaliyoridhiwa.

Mheshimiwa Spika, upungufu wa bajeti ya maendeleo; bajeti ya maendeleo haitoki kama inavyoombwa na kumekuwa na changamoto nyingi katika W izara hii na miradi ya sekta hii katika uwanja wa Taifa, wadhamini mbalimbali wamekuwa wakihudumia uwanjahuo wakiwemo Wachina ambao mkataba wao unaishia mwezi Agosti, 2018 na sportpesa mkataba wao mwisho mwezi Mei, 2018. Hata hivyo, hakuna mkakati wowote unaoonesha viwanja hivi vitashughulikiwa kwa kuwa hata bajeti haijajionesha wazi. Waziri anapohitimisha atueleze mkakati ukoje wa kuhakikisha uwanja huu umetunzwa ipasavyo.

Mheshimiwa Spika, nazidi kusisitiza kuwa na maandalizi mazuri ya michezo kuanzia under 17 kwa jinsia zote, kuwe na mkakati wa mafunzo maalum na maandalizi kwa timu zetu. Ahsante sana.