Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Katiba na Sheria

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Katiba na Sheria

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono hoja na ningependa kuchangia suala moja muhimu. Jimbo la Muheza halina jengo la Mahakama ya Wilaya, bajeti iliyopita ilikuwa limepangwa kwenye mpango wa ujenzi na likaondolewa katika hatua za mwisho, mwaka huu katika bajeti hii limeondolewa kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Muheza tulikwishatayarisha kiwanja muda mrefu, jengo linalotumika halina hadhi ya kimahakama, hivyo tunaomba tufikiriwe katika mpango wa ujenzi wa kisasa. Nakushukuru.