Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia kwenye mjadala ulio mbele yetu. Kabla sijasahau, Mheshimiwa Sware amezungumza sana kuhusiana na Ruaha mto mkuu kukauka, lakini nataka tukumbushane kama Wabunge kuna mwandishi wa kitabu anasema: “The Politicians don’t care about economics, and the economists don’t understand politics.”

Mheshimiwa Spika, ni kweli watu wamepongeza nia njema ya Rais ya kutaka wale watu walionyanyaswa kwenye maeneo mbalimbali jinsi ambavyo wametendewa vibaya, lakini vilevile kama viongozi ambao tunalitakia mema Taifa hili tusije tukaziacha faida za kiuchumi ambazo zinatokana na kutunza mazingira. Kwa hiyo, natamani wote kwa pamoja kama Wabunge hayo tuyaangalie, tusipige kelele tu watu wanapovamia maeneo ya utunzaji, hatuwezi kusahau eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, takwimu za mwaka 2009 katika sekta ya utalii zinaonesha mapato duniani, yaliyotokana na shughuli za utalii yalikuwa dola za Kimarekani bilioni 852, watalii waliosafiri duniani kote walikuwa zaidi ya milioni 800 na sekta hii ilitoa ajira zaidi ya milioni 255 duniani kote, hii ilikuwa ni asilimia 11 ya ajira duniani.Hii inaonesha jinsi gani sekta hii ilivyo na umuhimu na inaajiri watu wengi na inazalisha shughuli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kumbuka wakati huo Serikali ilijaribu kupanua wigo, lakini kama dunia nzima toka wakati huo, miaka kumi sasa imepita watu walikuwa milioni 800 wanaotalii, wakati huo nchi yetu ilikuwa na uwezo wa kuvutia watalii laki nane na kitu, Mahiga atanisaidia, alikuwa Waziri wakati huo.

Mheshimiwa Spika, lakini mpaka leo, pamoja na fursa nzuri tulizonazo katika nchi yetu, hatujaweza kufikisha watalii 1500, tunahangaika hangaika kwa sababu hatuna mipango endelevu, milioni moja na nusu hatujafikisha, tunahangaika kwa sababu hatuna mipango endelevu. Hatuna mipango endelevu kwa sababu hatu-plan kama Taifa.

Mheshimiwa Spika, katika Wizara hii, Waziri aliyekaa muda mrefu katika historia ya nchi hii ni Mheshimiwa Zakhia Meghji na huyu Waziri inasemekana alikaa muda mrefu katika Wizara hii kwa sababu alikuwa anawasikiliza wataalam. Nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo zina vivutio vingi sana, tungeweza kuwa-attract kwa sababu hawa watalii tunanyang’anyana na nchi zingine, lakini kwa bahati mbaya Wizara hii imekuwa ikibadilishwa Mawaziri ambao wanaenda wanakuwa kama ni wajuaji kuliko uhalisia.

Mheshimiwa Spika, tuna fukwe nyingi, katika nchi yetu hatuja-utilize, tuna maeneo mbalimbali hatujaya-utilize, wakati ule takwimu hizi zinatokea wataalamu walikuwa wamejua kwamba na World Bank ilikuwa imesema kwamba kwa sababu sekta hii inaajiri watu karibu laki tano kama tukikuza utalii, upande wa kusini tutakuwa mara mbili, kwa sababu kaskazini ndio iko zaidi. Kwa hiyo tukikuza kusini itakuwa mara mbili.

Mheshimiwa Spika, nazungumza kwamba Wizara hii, tumekuwa hatuko consistency watu wanaoingia, kwa sababu tumeenda kwa pamoja mradi wa REGROW alikuja Makamu wa Rais alikuja Iringa, akauzindua lakini kwa taarifa nilizonazo kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati, huu mradi wa REGROW unaonekana unasua sua na kuna dalili kwamba World Bank wame-pull off hata hiyo hela tena, haipo tena. Kwa hiyo ile mipango yote mizuri, ambayo tulitakiwa tukuze Mikumi, tukuze Ruaha tuuokoe mto Mkuu Ruaha mipango hii yote inakufa tena.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tunaanza kulalamika katika suala la Utalii kwa sababu mipango tunayopanga inakuwa sio endelevu, kila anayeingia kwenye Wizara ni kama yeye ndio anaanza anaacha mipango mizuri ambayo wengine wameanza. Mfano mzuri rafiki yangu Mheshimiwa Kigwangalla amekuwa na matamko mengi ambayo ni matamko ambayo yanaleta madhara, Twitter zake zinaleta madhara. Juzi ameenda kwenye TTB amevunja Bodi, tumesikia tena hiyo Bodi haijavunjika bado ipo. Kwa hiyo masuala haya wanafanya mambo ambayo hawafanyi utafiti, yana-disturb industry.

Mheshimiwa Spika, industry hii ni very delicate, hawa watalii waliokuzwa kutoka laki nane mpaka tulipofika imefanyika kazi kubwa sana ya kutangaza utalii huu. Sasa tunapokuwa hatuko consistency, hatufanyi kama ambavyo tume-plan, tunasababisha industry iyumbe na inaingiza uchumi mkubwa sana katika nchi yetu. Kwa hiyo niiombe Wizara itafakari kwa makini, ni namna gani inaweza kuiendeleza sekta hii.

Mheshimiwa Spika, tuna matatizo ya hospitality tunapozungumza masuala ya hospitality ina-involve mambo ya customer care, ina-involve mambo ya customer service, ina-involve hoteli zetu nyingi ziko sub-standard watalii hawaendi tu kwa sababu ya kwenda hotelini na kwao kuna hoteli nzuri, hoteli ziko sub-standard, watu hatujawa-train, watu wakifika hapa wanapata shida. Sasa hao watalii wataongezekaje? Watalii wakija hapa kwetu watakwenda kulala wapi, watakaa wapi, kama hiyo competition hatulingani na watu wengine duniani. Hilo nilitaka nizungumze kwa mapana.

Mheshimiwa Spika, takwimu ambazo zimetolewa na Wizara yenyewe, tatizo lingine kubwa ambalo limesababisha watalii Tanzania isionekane ni nzuri zaidi mambo ya usafi, hygine kunaonekana kuna uchafu, watalii wanalalamika, ni takwimu za Wizara yenyewe, kuna mambo ya usalama, kuna mambo ya infrastructure, haya mambo yote wanayolalamika yanasababisha utalii uwe wa hovyo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine nataka kuzungumza ambalo kwa masikitiko makubwa niseme katika Kamati tulipokuwa tuna-windup jana tulilipanga nalo lingeweza kuzungumzwa katika Kamati hii, kwa bahati mbaya halijazungumzwa, ambalo katika Kamati yetu tulipata malalamiko kuhusu unyang’anywaji wa mashamba makubwa. Hatuna tatizo na mashamba makubwa kunyang’anywa kwa mujibu wa sheria, lakini kuna mashamba makubwa katika Wizara ya Ardhi, pamoja na sifa nyingi ambazo Mheshimiwa Lukuvi hata mimi nimeshiriki kumpa, lakini suala hili la mashamba makubwa lina harufu fulani ya ukakasi, lazima tuelezane ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika mashamba makubwa haya, kwa mfano Mheshimiwa Sumaye…

T A A R I F A

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, sasa mimi nimemchafuaje hapa anavyosema? Nadhani anaenda haraka, kwani nimesemaje sasa, anasema nimemchafua, wapi? (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nimezungumza kwamba sina tatizo kabisa na mashamba makubwa kunyang’anywa kwa mujibu wa Sheria na taratibu kwa kufuata procedure. Nimetoa mfano mmoja, mimi sijagusa mashamba ya Jimboni kwake, nimetoa mfano kwamba Mheshimiwa Sumaye, alikuwa na shamba lake, alilipata kihalali, ameliendeleza mpaka wana-revoke lile shamba lake alikuwa na ng’ombe 200 kwenye shamba, alikuwa na kondoo 350, nyumba kubwa ya umwagiliaji, visima, go-down. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ameambiwa hajaendeleza, nasema unyang’anyaji huu, Rais kubadilisha hati ana mamlaka hayo, Rais anaweza akabadilisha sio tatizo, lakini ninachosema...

SPIKA: Aaah, muda umekwisha Mheshimiwa, dakika kumi zimekwisha.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, dakika nane mpaka sasa hivi nikisoma hapa, ziko dakika nane….

SPIKA: Malizia sentensi yako basi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, mpaka sasa hizi ukiangalia jinsi ambavyo mashamba hayo yamechukuliwa, akina MO, wameendeleza mashamba lakini wamenyang’anywa, ndio maana sisi, lazima, bila ubaguzi…….

(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walizomea)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Lazima bila ubaguzi, tulitaka Kamati ya Uchunguzi iundwe, kwa nini mnakataa kuunda Kamati ya Uchunguzi? Lazima Kamati ya Uchunguzi iundwe ili tuone uhalali wa mashamba hayo kunyang’anywa. (Makofi)