Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Magdalena Hamis Sakaya

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Kaliua

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nikushukuru sana kunipa nafasi hii niweze kuchangia kwenye Mpango wa Bajeti ambayo ipo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala afya. Tunashida kubwa sana sana ya huduma ya afya watumishi wa afya almost ni Tanzania nzima, kiukweli baadhi ya huduma zimeporeshwa na hata dawa zimeongezeka hospitalini lakini watu wanafika hospitalini hawapati kuudumiwa kutokana kwamba hatuna watumishi wa afya. Kwa hiyo, naomba kwenye Mpango wa Maendeleo ujao lazima Serikali iyakikishe tumepata Watumishi wa afya wa kutosha maeneo yote ya Taifa hili kwenye zahanati, zahanati moja inakuwa na wahudumu wawili au mmoja, tunasema tunapunguza vifo vya akinamama na watoto, tumeporesha zahanati, lakini mama anafika pale anajifungulia nje kwa sababu mhudumu ni moja akaangaike na wagonjwa wa kawaida, akaangaike na mama anayejifungua, ahaangaike na mama mwenye mimba ni shida, tunaomba Serikali ije na mpango namna gani kuwakikisha nchi nzima maeneo yote tunakuwa na wahudumu wa kutosha wa afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwenye mpango ujao uoneshe kabisa namna kuakikisha kwamba hospitali zote za rufaa na hospitali mikoa zinakuwa na vifaa tiba muhimu vyote kila hospitali iwe na CT Scan ya hali ya juu, x- ray ya kisasa, iwe na ultrasound ya kisasa na iwe na MRI ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Muhimbili saiv inafanya vizuri kwa sababu ina vipimo hivyo, lakini watu ni wengi na siyo wote wanaweza kuja Muhimbili, wengine wanapata shida huko mikoani walipo.

Kwa hiyo, ili kuwakikisha kwamba Watanzania wanapata vipimo watibiwe vizuri kwa kutokana vipimo vyao na uchunguzi wa kutosha kwenye mikoa yote wahakikishe kwamba kuna vifaa tiba vya kutosha na tuhakikishe hili kwamba tunalinda afya ya Watanzania na watatibiwa siyo kwa kubahatisha bali kuhakikisha wamepata vipimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la utafiti, kiukweli katika miaka yote tunashauri hapa Bungeni hata kuingia mikataba na mataifa mengine kuweza kutenga fedha asilimia kumi ya pato la Taifa kwenda kwenye utafifi bado hatujaweza kufanya kama Taifa, huwezi kuwa na maendeleo endelevu bila kuwekeza kwenye utafiti. Ili uende kwenye kilimo vizuri lazima utafiti, ufugaji utafiti, uvuvi utafiti, huwezi leo suala la kilimo limezungumziwa sana siwezi kulizungumzia, lakini leo ukiangalia wakulima wengi wanalima kwa kubahatisha tunahitaji utafiti kwenye kilimo, utafiti kwenye pembejeo, utafiti kwenye mbolea, kwenye udongo, kwenye masoko kila kitu ni utafiti, kwa nini Serikali aitengi fedha asilimia moja kwenda kwenye utafiti? Kwa hiyo, mpango ujao uoneshe namna gani tunatenga fedha one percent la pato la Taifa kwenda kwenye utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine tunaomba kwenye mpango ujao uoneshe namna gani ya kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami, mikoa yote kwa barabara za lami mpaka sasa hivi kuna baadhi ya mikoa ambazo hakuna barabara za lami hazijaunganishwa mkoa kwa mkoa barabara za lami kwa sababu nchi yetu ni nchi ya kilimo wakulima wanapata shida sana kusafirisha mazao kutoka kwenye mkoa mmoja kwenda kwenye mkoa mwingine hakuna barabara za lami, leo kule Kaliua unakuta kuna mahindi ya kutosha, lakini mkoa mwingine kuna shida ya mahindi, kuyapeleka inakuwa ni shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuhakikishe kwenye mpango ujao namna gani ya kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania na kwa barabara za lami, kwa mfano, Kaliua kuna barabara inayoanzia Katavi inakuja Kaliua inakuja Kahama inakwenda mpaka Rwanda, leo tuna mahindi ya kutosha Katavi, mahindi ya kutosha Kaliua lakini Rwanda wanahitaji mahindi barabara ingekuwepo ya kutosha imeunganishwa ingeweza kusafirisha masoko huko kuliko kutegemea pale pale au pale ndani ya mkoa kwa hiyo lazima mpango ujao uoneshe hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine tunakwenda kwenye uchumi wa kati lakini uchumi wa viwanda, hatuwezi kuwa na uchumi wa viwanda kama hakuna umeme wa uhakika na kutosha tena umeme wenye nguvu. Ni ukweli REA inajitahidi kuweza kusambaza umeme lakini ule umeme una nguvu ndogo, transfoma zilizowekwa ni ndogo, mvua ikinyesha ime-shake hakuna, unakuta hata viwanda vidogo ambavyo viko size ya welding, kusukasuka na kunyoa bado wale vijana hawafanyi kazi kwa uhakika kutokana umeme hauna uhakika. Kwa hiyo, kwenye mpango ujao wa bajeti lazima tuhakikishe namna gani tunakuwa na umeme wa uhakika, tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda huwezi kuzungumzia viwanda kama umeme ni wa aina hii ambao tunao sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali ije na mpango namna gani ya kuhakikisha kwamba tunajenga substation zote za kupokelea umeme na kusambaza umeme, kwa mfano pale Kaliua na Urambo kuna sehemu ya kujenga substation, ilikuwa kwenye mpango wa bajeti uliopita tunaomba itekelezeke ili tuweze kupata umeme wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala mazingira pamoja na mabadiliko ya tabianchi. Nimeangalia kitabu cha Mheshimiwa Waziri kina sentensi moja tu inayoonesha suala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, hili suala la mazingira, hili suala la mazingira ni suala gumu na ni suala ambalo ni very serious, lakini kiukweli Serikali haijawekeza kwenye mabadiliko ya tabianchi na kupambana na mazingira kabisa na hata ukiangalia kwenye bajeti zilizotangulia mwaka juzi/mwaka jana fedha inayotoka kwenye bajeti ya Wizara ya Mazingira ni kidogo sana asilimia kubwa inakwenda Muungano lakini bajeti ya mazingira ni kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania imeshakuwa bare maeneo mengi, misitu inazidi kuteketea, mbao zinaondoka, lakini hakuna mkakati lakini tuna desasters, tuna matetemeko ya ardhi, tuna baadhi ya visiwa vinazama, yapo matukio mengi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, lakini hatuoni fedha inatengwa na ukiangalia fedha inayotengwa kwenye bajeti za nyuma ni fedha ya nje kwa maana fedha ya ndani haitengwi ya kutosha na wakati mwingine haitengwi kabisa, lazima mpango ujao uoneshe namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutunza mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nategemea sana mojawapo ya kitu kinachopoteza sana misitu ya Tanzania ni suala la uchomaji wa mkaa na Mawaziri wanaona wakipita kutoka Dodoma kwenda Morogoro, kwenda Dar es Salaam tunategemea makaa ya mawe itakuwa ni solution kutoa nishati kupunguza kukata mikaa kwenye miti, kuharibu misitu, lakini ukiangalia huku Mheshimiwa Waziri anasema makaa ya mawe, basi Serikali inaangalia kama mwekezaji huyo atakuwa na manufaa kwa Taifa. Miaka 20 kweli Serikali inaangaliaga tu? Miaka 20 makaa tunayo hapa hapa tuweze kuyatoa ni kuya-export na kuyatumia, lakini tunakuwa jagwa huku tunasubiria tunasubiria tunachukua muda mrefu sana kutekeleza mradi wa kimkakati ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hili suala la mazingira liangaliwe na huu mradi wa makaa ya mawe upewe kipaumbele cha kutosha ili tuweze kutumia nishati mbadala ili tuokoe misitu inayoteketea na tuweze kulitoa Taifa hili kwenye jangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine tumekuwa tunaomba sana Serikali tuwe na vikosi makini vyenye uwezo wa kuweza kuokoa kwenye vyombo vya maji. Tumeona kipindi hiki jinsi tumepata shida, watu wameteketea kwa sababu hatuna kikosi makini cha kuokoa, tumeomba miaka mingi kwamba lazima kama Taifa kwenye vyombo vya maji, kwenye ukanda wa maziwa yote na ukanda wa bahari tuwe na vikosi makini vya kuokoa, lakini leo watu wamezama kwenye maji, tunaenda kutumia wavuvi siku mbili/tatu mpaka wengine wamepoteza maisha kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba kwenye mpango ujao Serikali iweke mkakati na mpango namna ya kuwa na vikosi makini vyenye uwezo na vifaa na weledi wa kutosha kuweza kusaidia kuokoa watu pale inapotokea tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine suala la mifugo tunaiomba bajeti ijayo au mpango ujao uonyeshe vizuri namna gani ya kutumia rasilimali ya mifugo ya Taifa hili kuweza kuongeza uchumi wa Taifa kwa kiasi kinachotosha lakini pia kuweza kusaidia uchumi wa jamii ya wafugaji na Watanzania kwa ujumla. Pamoja na kuwa tuna rasilimali ya mifugo lakini bado hatujaweza kuitumia vizuri. Tunaomba bajeti ijayo ioneshe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mifugo, ioneshe viwanda kwa ajili ya mazao ya mifugo, ioneshe ruzuku ya Serikali kwa ajili ya kusaidia kwa ajili ya kusaidia mifugo...

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana ahsante.