Parliament of Tanzania

Mhe. Spika awahamasisha Wabunge kwenda AFCON

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amewahamasisha Waheshimiwa Wabunge wote kujiandaa kwa ajili ya kwenda kuipa hamasa Timu ya Taifa wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika zinazotarajiwa kuanza mwezi Juni 21 mwaka huu nchini Misri.

Akizungumza Bungeni Mhe. Spika amesema kuwa itakuwa ni jambo la aibu iwapo Wabunge wa nchi nyingine za Afrika Mashariki ambao timu zao za Taifa zimefuzu watajitokeza kwa wingi alafu Wabunge kutoka Tanzania wasionekane.

“Ni fusra ya pekee ambayo haijawahi kutokea kwa hivyo nawaombeni tujitahidi kujiandaa kwenda na mimi nitaangalia kama kuna uwezekano wa kupunguza baadhi ya gharama ili muweze kwenda kwa wingi,” alisema Mhe. Spika.

Mhe. Ndugai aliongeza kuwa mawasiliano yanaendelea kufanyika na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili iweze kuratibu safari ya Waheshimiwa Wabunge kwenda huko Misri kwa kwa ajili ya fainali za AFCON.

“Mpaka sasa inaonekana ukiwa na dola za Kimarekani kuanzia 1,500 unaweza kugharamia safari pamoja na malazi,” alisema Mhe. Spika nakusisitiza kuwa angependa Wabunge wote waende kwani watapata pia fursa ya kufanya utalii wakiwa huko nchini Misri

Timu ya Taifa ilifuzu kwenda kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 kwa kushika nafasi ya mbili katika kundi lao mara baada ya kuifunga Uganda magoli 3-0 katika mchezo wake wa mwisho.

Katika fainali hizo za mataifa ya Afrika Timu ya Taifa imepagwa katika kundi C pamoja na timu za Taifa za Senegal, Algeria na Kenya.

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

Member of the Parliament

View All MP's