Parliament of Tanzania

Mhe Spika atembelea Bunge la Kenya

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge,Mhe Mary Chatanda,Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.

Aidha akizungumza alipokutana na Spika Wa Bunge la Kenya Mhe Ndugai amesema kuwa alipokea mwaliko wa kutembelea Bunge la Kenya kutoka na historia kubwa ambayo mabunge yote mawili yanao.

"Mabunge yetu mawili yamekuwa na ushirikiano mkubwa kwa miaka mingi," alisema Mhe Ndugai.

Kwa upande wake Spika Wa Bunge la Kenya Mhe Muturi alisema "tumefurahi kwa kukubali mwaliko wetu na kuambatana na wabunge.Kupitia ziara yako nina imani sote wawili tutajifunza mengi katika uendeshaji Bunge hususan kwa mabadiliko ambayo hapa Kenya tumefanya".

Hon. Job Y. Ndugai

Speaker of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Mr. Stephen Kagaigai

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's