You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Abdulla, Amina Amour[CUF]

Special Seat
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
6 101 EAST AFRICAN CO-OPERATION East Africa Co-operation 9 February 2012
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali moja la nyongeza. Je, Mheshimiwa Waziri utaratibu uliotuelezea kuhusiana na mchakato mzima wa kupitisha miradi hii. Je, uko sawa baina ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  101  SESSION #  6
mp Answer From Hon.Saadalla, Dr. Abdulla Juma Abdulla
EAST AFRICAN CO-OPERATION
NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Amina Abdallah Amour, la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki inahusisha Tanzania kuwa kama ni nchi ya partner state. Kwa kuwa Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na Tanzania Bara ni wazi kwamba huu utaratibu unahusisha sehemu zote mbili. Kwa taarifa yake Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Zanzibar kwamba kule Zanzibar kuna ZCIA ambayo ndio inaratibu upatikanaji wa Certificate za Original.

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii niongezee kidogo juu ya majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Naomba nitoe taarifa tu kwa wafanyabiashara wanaotoka hususan Pemba, kuelekea Mombasa, Serikali ya Kenya imetuletea kama Tangazo hivi la tahadhari kwamba wao hivi sasa wako vitani wanapambana huko Somalia.

Kwa hiyo, wafanyabiashara wanaokwenda Mombasa Shimoni wazingatie kwamba haitakuwa rahisi kutambua maadui hasa nyakati za usiku. Kwa hiyo, wanashauriwa waweze kwenda saa za mchana na biashara zao itakuwa vepesi zaidi.

Kwa hiyo, tumepata tatizo la wavuvi 51 kukamatwa kule Mombasa na hao wametoka Pemba, lakini tumelishughulikia na Ofisi ya Ubalozi Mdogo pale Mombasa tumeweza kulipa faini na wavuvi 51 wote Watanzania wale wamerejeshwa bila tatizo lolote. Lakini sasa tuchukue tahadhari.