You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Soni, Jitu Vrajlal[CCM]

Babati Vijijini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
10 101 AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES Irrigation 7 February 2013
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza. Je, ni lini Serikali itatatua tatizo kama hili la Lower Moshi kukosa maji na kwa kuwa Serikali ni moja Wizara zote zinazohusika iwe ya Maji, Kilimo na Wizara ya Mazingira wakae pamoja na kubuni namna ya kuhakikisha kwamba wanaweka mipango pamoja ili ukosefu wa maji isitokee na ni kwa Tanzania nzima na isiwe kwenye eneo moja tu la Lower Moshi tu?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  101  SESSION #  10
mp Answer From Hon.Malima, Adam Kighoma Ali
AGRICULTURE, FOOD SECURITY AND CO-OPERATIVES
NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nimshukuru Mheshimiwa Jitu Soni kwa sababu ametambua kwamba tatizo hili sio tatizo la mtu mmoja.

Ni tatizo la maji ni tatizo la Mazingira tatizo la TAMISEMI na kama walivyokuwa anazungumza Mheshimiwa Mwanri wakati wa kujibu hapa dakika zilizopita na kama nilivyozungumza juzi wakati najibu swali la Maliasili na Utalii la Bonde la Usangu ni lazima sisi Watanzania wote tujue kwamba kadiri tunavyoendelea kuharibu vyanzo vya maji, tunavyoharibu ardhi hizi wet lands na kadhalika. Tutafika sehemu ambayo vyanzo vya maji vitateketea tu. Tutakuwa hatuna hata maji ya skimu za irrigation.

Kwa hiyo, mimi nadhani hili ni tatizo ambalo Serikali tumejipanga na nadhani katika kulikabili itabidi tulianzie humuhumu Bungeni ili sisi wenyewe tupate ufahamu wa majukumu yetu na wajibu wetu wa pamoja katika kukabiliana na tatizo hili leo ili tusianze kuulizana maswali miaka kumi na tano wakati tutakapokuwa tumekosa maji kabisa katika vyanzo vyote vya irrigation.