You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Jumaa, Hamoud Abuu[CCM]

Kibaha Vijijini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
7 113 WORKS Communication/Infrastructure 20 April 2012
Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri ambayo yana masikitiko
makubwa ameainisha barabara ambazo hazipo katika Jimbo langu,
lakini majibu haya ya upembuzi yakinifu tumechoka nayo sasa.
Tunahitaji utekelezaji wa barabara hii ya Makofia –Mzenga ni
barabara ambayo inategemewa na wananchi wa Jimbo la Kibaha Vijijini
katika kunyanyua uchumi wa Jimbo lao. Ni lini sasa barabara hii
itajengwa kwa kiwango cha lami?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  113  SESSION #  7
mp Answer From Hon.Mwakyembe, Dr. Harrison George
WORKS
NAIBU WAZIRI WA UJENZI:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri
wa Ujenzi, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abuu, kama
ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge
kwamba hatutaweza kuijenga hiyo barabara bila kufanya upembuzi
yakinifu na pia usanifu wa kina. Tuko kwenye kipindi cha sayansi na
teknolojia, hatuwezi kurudi tena enzi zile za kuweka kamba na kuanza kulima barabara bila hata kufanya upembuzi yakinifu. Tumepanga
kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na pesa tutakuwa tunayo
katika kipindi cha mwaka 2013/2014.