You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Makalla, Amos Gabriel[CCM]

Mvomero Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 106 INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING Industry 23 June 2011
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ambayo hayajajitosheleza swali langu. Lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Naibu Waziri alivyojibu si kweli kwamba kiwanda cha Mtibwa kimewahi kuzalisha sukari tani 50. Hizo ni takwimu za uwongo kwa hiyo, amejibu uwongo. Kwa sababu, takwimu nilizonazo…

Mheshimiwa Spika, ahsante. Takwimu za ukweli tulizonazo ni kwamba mpaka mwaka jana, tangu kiwanda kibinafsishwe mwaka 1997, kiwanda kimezalisha tani 40,000 na sasa matarajio ya mwaka huu ni tani 47,000 kwa hiyo, hakijawahi kuzalisha tani 50,000. Kwa hiyo, ninayo orodha hapa na uzalishaji wa tani kwa kila mwaka mpaka mwaka jana?

(a)Mheshimiwa Spika, swali; kwa kuwa, Serikali inasema kwamba kwa kuanzisha kiwanda kingine tutakuwa tunakiuka sheria. Serikali haioni kwamba kwa kero zilizopo katika kiwanda cha Mtibwa, ndio kitaendelea kuwadidimiza wakulima? Kwa sababu, zipo kero za kuchelewesha mishahara, kulipa bei ndogo ya sukari?

(b)Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ipo haja sasa ya kuwawezesha watanzania wenye nia ya kuwekeza kiwanda kingine. Na kwa kuwa, lipo dirisha la wakulima kupitia benki ya TIB na fedha nyingine ziliwahi kuongezwa hata za EPA.

Je, Serikali sasa haioni kwamba ipo haja ya kuondoa monoksoni iliyopo kiwanda cha Mtibwa, ili kuwawezesha wazawa na wananchi wengine kuweza kuweka kiwanda kingine na kuondoa kero hizi nilizozitaja?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  106  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Nyalandu, Lazaro Samuel
INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA:

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Makalla, kwa juhudi zake na jitihada zake za kuwatetea wakulima wa miwa katika eneo hili la Mtibwa, kule kule Morogoro.

Mheshimiwa Spika, katika jibu la msingi ambalo nimelitoa Serikali imesema kwamba kiwanda hiki cha sukari kina kitu kinachojulikana kwa kitaalam installed capacity ya tani 50,000. Na hatujasema kwamba kinazalisha tani 50,000.

Mheshimiwa Spika, la pili Katika jibu la msingi tumesema, uzalishaji wa miwa uliopo katika hili eneo la Mtibwa, kwa wakulima wote wadogo wadogo ni tani 38,000. Kwa maeneo mengine uzalishaji wa miwa ni mdogo kuliko installed capacity na chini ya Kanuni za sukari zinazosimamiwa na Bodi ya Sukari, ni lazima kwanza kiwanda kilichoanzishwa kiweze kukidhiwa mahitaji ya kuwa na uzalishaji wa kutosha kabla ya kiwanda kingine hakijaruhusiwa. Utaratibu unaotumika kuruhusu uanzishwaji wa kiwanda kingine ni sharti kiwe umbali wa kilometa 80 kutoka kiwanda kilichopo cha kwanza. Lakini la pili, ni lazima mahitaji halisi ya kiwanda cha kwanza yawe yametimizwa na kuwe na uwezo kiukulima wa kuweza kutoa miwa yakutosha kwa ajili ya kiwanda cha pili.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge, kwa kuendelea kuwahimiza wananchi wake, kuwa tayari kuanzisha kiwanda cha sukari, TIB, katika dirisha la kilimo. Serikali itaendelea kuwa tayari kuwasaidia na wakati muafaka wa ukulima huu utakapoongeza capacity, Serikali itawaunga mkono katika juhudi hizo.