| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 5 | 50 | JUSTICE AND CONSTITUTIONAL AFFAIRS | Justice/Constitution | 11 November 2011 | ||
| Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ruhusu yako, pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria naomba nimwulize maswali mawili madogo yafuatayo: Pale IMTU au Herbert Kairuki kama mifano y huduma za jamii watoto wa wakulima mara nyingi wanalalamika kwamba wanapata taabu sana kulipa kwa kufuata dola na kwa kufuatia dola inavyopanda na kwamba wanashindwa kulipia gharama za masomo ipasavyo na kwa mara kadhaa imekuwa inawadhalilisha kwa sababu wanashindwa kusoma hawajalipa na hawaingii darasani. Sasa hizi gharama ni kubwa je, Serikali haioni kwamba umefika wakati wa kuachana kabisa na mtindo wa kusaini mikataba ambayo inasisitiza dola au sarafu ya kigeni na kuwadhalilisha wananchi? Pili, hii mikataba ya dola hasa ya kimarekani ambayo inatiwa saini pale. Serikali haioni kuwa yaweza kuwa ni cheche ya kuweza kuwasha moto wa migomo? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 50 SESSION # 5 | ||||||
|
||||||
| WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mikataba mbalimbali kutozwa kwa dola. Hiyo kama Serikali tuna discourage ni vyema mara nyingi ikatumika fedha yetu shilingi badala ya kutumia dola na hata katika hotel mbalimbali ni vyema na ni busara ikatumika shilingi yetu. Kwa hiyo, suala la IMTU linashughulikiwa na Serikali kwa upana wake, tunaangalia ni jinsi gani tunaweza tukawasaidia wale wanafunzi wa IMTU. Saula la kuchochea migomo. Migomo inachochewa na sababu mbalimbali sio suala la dola peke yake. Kwa hiyo suala la migomo sio suala jema na si suala zuri. Ni vyema watu tukamaliza matatizo yetu kwa njia ya maelewano badala ya njia ya migomo. |
||||||