| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 10 | 113 | FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS | Tax | 8 February 2013 | ||
| Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niulize swali moja tu la nyongeza kama ifuatavyo:- Kwa kuwa kumekuwa na sintafahamu katika ukusanyaji wa mapato katika nchi yetu, hali inayopelekea Watanzania kutoamini kuwa mapato haya yanayopatikana siyo sawa. Je, Serikali inawaambiaje Watanzania kuhusu hali hiyo? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 113 SESSION # 10 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhani Haji Saleh, Mbunge wa Bumbwini, kama ifuatavyo:- Ningependa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kuwa, takwimu tunazozitoa kwa ajili ya kulipa kodi zipo wazi na mahali popote pale ambapo kodi inapokelewa kuna taratibu zake na takwimu zinawekwa. Kwa hiyo, labda kitakachotakiwa ni kuwa zioneshwe kwa uwazi zaidi, sehemu nyingi zaidi, ili Wananchi waamini kama kweli tunapokea hizo kodi kama tunavyotamka na kuwa kodi hizo zinatumika katika maeneo ambayo Serikali imepanga kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi. Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna mengine zaidi tutajitahidi kadiri iwezekanavyo, kutoa taarifa zaidi mpaka kufikia walengwa wote hadi Wananchi wa Vijijini kujua kama kweli tunakusanya, lakini takwimu hizo ni sahihi na ni rahisi kuzithibitisha. |
||||||