You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Haji, Khatib Said[CUF]

Konde Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
9 110 VICE PRESIDENT'S OFFICE (UNION AFFAIRS) Union Affairs 9 November 2012
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, napenda kujua, kuna utaratibu kwa wageni wote au watu wote wanaotoka nje ya nchi hii wanapotaka kuingia Tanzania kwa kutumia usafiri wao, wanaruhusiwa kuingia hapa kwa kutumia kitu kinachoitwa foreign permit.

Je, kuna utaratibu gani kwa Mzanzibari au Mtanzania kutoka Zanzibar anapotaka kuingia na gari yake hapa ambayo kwa sasa inavyoelezwa Mzanzibari analazimika kuweka deposit ili aweze kuingia na gari yake katika nchi yake mwenyewe ya Tanzania?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  110  SESSION #  9
mp Answer From Hon.Suluhu, Samia Hassan
VICE PRESIDENT'S OFFICE (UNION AFFAIRS)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO:

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu awali kwamba moja katika changamoto tunazozipata katika Muungano ni suala la usajili wa vyombo vya moto.

Ni kweli kwamba gari zinazotoka Tanzania Bara zinaingia Zanzibar bila kuulizwa lakini Sheria zilizopo Tanzania Bara zinahesabu gari zinazotoka Zanzibar ni kama gari za kigeni.

Suala hili limekuwa changamoto kwa siku nyingi na kama nilivyosema kwamba tumelifanyia kazi, tulifikia pahali kurekebisha sheria zilizopo, kwa Zanzibar imekuwa rahisi kurekebisha Sheria zilizopo lakini kwa upande wa Tanzania Bara suala hili linashughulikiwa na vyombo vinne; Ujenzi, Mambo ya Ndani na vyombo vingine.

Kwa hiyo, tumeamua kwamba Wizara ya Ujenzi watunge sheria mpya itakayofanya marekebisho yale ambayo yanawakera upande wa pili wa Muungano, hatua hiyo sasa inatekelezwa. Tayari Sheria mpya iko katika kutungwa na Wizara ya Ujenzi.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mbunge wa Konde, kama ifuatavyo:-

Kama nilivyojibu awali kwamba moja katika changamoto tunazozipata katika Muungano ni suala la usajili wa vyombo vya moto. Ni kweli kwamba gari zinazotoka Tanzania Bara zinaingia Zanzibar bila kuulizwa, lakini Sheria zilizopo Tanzania Bara zinahesabu gari zinazotoka Zanzibar ni kama gari za kigeni.

Suala hili limekuwa changamoto kwa siku nyingi na kama nilivyosema kwamba tumelifanyia kazi, tulifikia pahali kurekebisha Sheria zilizopo, kwa Zanzibar imekuwa rahisi kurekebisha Sheria zilizopo lakini kwa upande wa Tanzania Bara suala hili linashughulikiwa na vyombo vinne; Ujenzi, Mambo ya Ndani na vyombo vingine.

Kwa hiyo, tumeamua kwamba Wizara ya Ujenzi watunge Sheria mpya itakayofanya marekebisho yale ambayo yanawakera upande wa pili na hatua hiyo sasa inatekelezwa, tayari Sheria mpya iko katika kutungwa na Wizara ya Ujenzi.