| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 6 | 100 | EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING | Education | 9 February 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika nashukuru sana. Kwa kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni matokeo ya shule zetu yameendelea kushuka na mifano halisi ni mwaka jana katika matokeo ya shule za msingi na mwaka huu katika matokeo ya Kidato cha Nne. Je, Serikali sasa inaweza kutueleza tafsiri ya matokeo haya na thamani ya elimu ya Tanzania inakoelekea? | ||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 100 SESSION # 6 | ||||||
|
||||||
| WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, tumepata kadhia kubwa hasa kuanzia mwaka jana kwa matokeo ya Kidato cha Nne, yale yalikuwa siyo mazuri kama tulivyotegemea. Lakini jambo la uhakika ni kwamba tumechukua hatua kubwa ya kuongeza nafasi katika elimu ya Sekondari ama access kwa kiwango kikubwa kushinda nchi yeyote katika Bara la Afrika kwa miaka ya hivi karibuni. Bila shaka unapochukua hatua kubwa kiasi hicho kutajitokeza madhara upande mwingine. Tuliyatambua hayo na matokeo yake ni haya ambayo tumeyaona mwaka jana ya wanafunzi wengi kutokufanya vizuri. Mheshimiwa Spika, naomba nilihakikishie Bunge lako Tukufu kwamba Serikali imejipanga kimadhubuti kuhakikisha sasa baada ya kulishughulikia tatizo la access sasa tunapanda kwenye ubora wa elimu na ndiyo nia thabit ya mpango wa maendeleo ya elimu ya Sekondari awamu ya pili, haitoangalia kujenga majengo tena, inakwenda kwenye ubora wa elimu. Hatua zote tutakazozichukua kwa maana ya Walimu, kumalizia madarasa ambayo hayajaisha, kujenga maabara, na kujenga maktaba na kuweka vitabu, yote hayo na mengine mengi yanalenga katika ubora wa elimu kama tulivyoona mwaka huu 2012 mtihani matokeo yake yamepanda walau kwa asilimia ndogo. Sasa ufaulu ni asilimia 52 tofauti na mwaka jana asilimia 50. Lakini kuanzia sasa na kuendelea bila shaka Bunge hili litaona mabadiliko makubwa katika shule zetu za Secondary ziwe Functional Secondary Schools. |
||||||