| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 4 | 12 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 8 June 2011 | ||
| Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa niaba ya wananchi wa wilaya na jimbo la Kishapu kwa kuwa sisi hatuna kabisa chumba cha kuhifadhia maiti, hatuna hospitali ya wilaya. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwasogezea wananchi wa jimbo la Kishapu hospitali kwa taabu wanazozipata hasa akina mama Mheshimiwa Spika kama wewe wanapata taabu kwa kusafiri kilomita zaidi ya 150 kwenda kujifungua Shinyanga Mjini? Naomba Mheshimiwa Waziri anihakikishie hapa. Je, haoni umuhimu wa afya za wanawake na wananchi wa jimbo la Kishapu kupata huduma ya hospitali ya Wilaya? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 12 SESSION # 4 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Suleiman M. Nchambi, Mbunge wa Kishapu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri Kishapu yenyewe nimefika sijui kama wakati ule mheshimiwa alikuwa ni Mbunge, nafikiri yeye ni mpya. Analosema hapa ni kweli jana nilikuwa najibu swali hapa kuhusu hospitali za wilaya, wilaya hizi mpya zinazoanza sasa hivi ukisema kwamba zote kwa mpigo utazipa hospitali za wilaya it is impossible, haitawezekana. Nilichosema jana maoni ya serikali ni kwamba hebu kila wilaya mpya itafute mahali ambapo tutaanzia katika kipindi cha mpito. Useme hapa kwenye kituo cha afya ndipo tutakapopatumia kama hospitali ya wilaya mpaka hapo tutakapokuwa tumefika mahali ambapo tunajenga hospitali ya wilaya, hivyo ndivyo ninavyoamini kwamba inaweza ikasaidia na ndivyo Serikali inavyoamini. Kwa hiyo, ninachomwomba Mheshimiwa Mbunge wa Kishapu wao wa-identify ili waweze kupewa ile heshima inayolingana na hospitali ya wilaya wakati tunaendelea kusaidia jambo hilo. Mheshimiwa Spika, isisahaulike hapa kujenga hospitali ya wilaya unazungumza habari ya bilioni tisa (9). Kwa hiyo, ninachosema hapa amezungumza habari ya akina mama; akina mama ndio wanaotuleta hapa duniani, mimi siwezi kusimama hapa nikasema kwamba tusiwasaidie akina mama, akina mama wasaidiwe na tuwasaidie kwa utaratibu na sisi wote tunaona umuhimu huo. |
||||||