| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 3 | 14 | NATURAL RESOURCES AND TOURISM | Tourism/Natural Resources | 5 April 2011 | ||
| Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipatia fursa ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri, kabla ya kuuliza swali ni kwamba, kwenye majibu yako umesema Wilaya ya Kasulu na swali langu lilikuwa ni Wilaya ya Kibondo. (i) Serikali ina juhudi gani za kupima upya maeneo ya hifadhi na kuwaruhusu Watanzania kuanza kuwinda kwenye maeneo hayo kwani kuruhusu wageni peke yao ni suala la ukoloni mamboleo? (ii) Tumekuwa tunapoteza mabilioni ya shilingi kutokana na Serikali kushindwa kutoza kodi hoteli za kitalii zilizoko kwenye mbuga hizi. Sasa Serikali ina mpango gani wa kufuata ushauri wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili tuweze kunufaika na pesa hizi? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 14 SESSION # 3 | ||||||
|
||||||
| WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mkosamali kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, mwaka juzi Bunge lako Tukufu lilipitisha Sheria Namba 5 ya Mwaka 2009, inayosimamia Sekta ya Wanyamapori. Katika Sheria hiyo, tulianzisha utaratibu wa kuwepo kwa Wildlife Management Areas kwenye maeneo ambayo yako nje ya core protected areas, yaani nje ya Game Reserve na National Parks. Kwa maeneo kama haya ya Makere ambayo yako nje ya core protected area, kwa maana ya Muyowosi Game Reserve, Wananchi wa maeneo hayo wanashauriwa kuanzisha Wildlife Management Areas ili waweze kuyasimamia wenyewe na kwa kufanya hivyo inakuwa ni rahisi kwao kupata user right na kuweza kupata mapato. Aidha, niseme tu kwamba, katika zoezi ambalo tumekamilisha hivi sasa na tumekwisha kutangaza, la vitalu vya uwindaji wa kitalii, kuna maeneo ambayo tumetenga kwa ajili ya wawindaji wenyeji. Katika jumla ya vitalu 172 ni vitalu 156 tu ambavyo vimetangazwa kwa ajili ya uwindaji wa kitalii, vitalu vitano ni kwa ajili ya utafiti pamoja na mafunzo na vitalu vingine vinavyobaki ni kwa ajili ya wawindaji wenyeji pamoja na utalii wa picha. Kwa maana hiyo, kuna maeneo maalum kabisa ambayo yametengwa kwa ajili ya wawindaji wenyeji. |
||||||