You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Kahigi, Prof. Kulikoyela Kanalwanda[CHADEMA]

Bukombe Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 109 LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT Livestock 23 June 2011
Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniruhusu kuuliza maswali mawili ya nyongeza, katika nchi nzima ya Tanzania katika miaka ya karibu kumetokea ongezeko la mifugo ambayo katika hali ya kawaida ni neema lakini ongezeko hili ni tatizo kubwa na namwuliza Waziri au tuseme Serikali. Je, inaonaje kama ingeunda jopo la wataalam ili wafanye utafiti na kuishauri Serikali kuhusu tatizo hili kwa sababu ni tatizo kubwa?

Je, Mheshimiwa Waziri amesema kwamba zoezi la kuwatengea sehemu ya malisho wafugaji linaendelea, je, zoezi litafanyika katika jimbo la Bukombe?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  109  SESSION #  4
mp Answer From Hon.David, Dr. David Mathayo
LIVESTOCK AND FISHERIES DEVELOPMENT
WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Prof. Kulikoyela Kahigi, Mbunge wa Bukombe, kama ifuatavyo. Swali la kwanza alilouliza kusema kweli kuongeza kwa mifugo ni dalili nzuri na ni opportunity ambayo Watanzania tunatakiwa tuitumie ili mifugo hiyo iweze kuongeza pato la taifa na kubadilisha maisha ya wafugaji. Lakini kuhusu kuunda chombo ama jopo la wataalam kuchunguza kuongezeka kwa mifugo sidhani kwamba hii inahitaji kuundwa tume, kinachotakiwa ni kwamba wafugaji waelewe kwamba hii ni rasilimali yao ya kuwasaidia na waweze kujisaidia kuvuna mifugo hiyo ili isiweze kuharibu mazingira. Katika sheria yetu ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo Na. 13 ya mwaka 2010 tunasisitiza kwamba wafugaji wafuge kutokana na eneo walilo nalo na tabia za kuhamama si nzuri na wala siyo suluhisho la kuweza kutatua matatizo ya ardhi tuliyonayo. Wafuge wanyama ambao wanalingana na eneo lao. Serikali kupitia DADPs na program zingine itakuweka miundombinu kwa ajili ya mifugo yao.