You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Amer, Abdulsalaam Selemani[CCM]

Mikumi Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
4 243 ENERGY AND MINERALS Energy 15 July 2011
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri yenye matumaini. Kuna taasisi moja ya kidini ina mpango wa kujenga au kutumia maporomoko ya Mto Yuvi kwa ajili ya kutoa umeme kwenye Kata ya Kisanga.

Je, Serikali iko tayari kushirikiana na taasisi hiyo ya kidini ili waweze kupata msaada wa Serikali waweze kutoa umeme kwa ajili ya Kata ya Kisanga na Kata iliyoko jirani na Kata ya Kisanga?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  243  SESSION #  4
mp Answer From Hon.Malima, Adam Kighoma Ali
ENERGY AND MINERALS
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdulsalaam kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iko tayari kushirikiana na waendelezaji na hiyo taasisi ya kidini kwa sababu hiyo inaendana na malengo ya kuanzishwa kwa REA.

Kwa hiyo, ninaomba tuwasiliane na hao watu wa taasisi ya kidini waje Wizarani tuwaelekeze REA ili kwa pamoja wafanye tathmini wajue kama kwenye hayo maporomoko panaweza pakapatikana umeme wa kutosha kwa bei nafuu yenye ufanisi kwa hizi Kata zote ambazo zimekusudiwa.