| E-mail this to a friend | Printable version |
|
||||||
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 6 | 31 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 2 February 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, mpaka sasa wanaodai ni wananchi 720 lakini Halmashauri imekuwa inawapiga chenga. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kuunda Tume na kuchunguza suala hilo kwa sababu mpaka sasa Serikali inasema imewalipa, watu 720 wakati hawajalipwa? Je, haya malipo yamekwenda wapi? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 31 SESSION # 6 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdul – Aziz Mohamed Abood, Mbunge wa Morogoro Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, jana wakati najibu maswali hapa nilisema kwamba kamwe Serikali hatutapuuza jambo lolote ambalo linaletwa mbele yetu na Mheshimiwa Mbunge. Mimi nataka nimpe takwimu hizi nitakazompa na yeye ata-compare na kama anahitaji sisi tuunde tume au twende kule sisi wenyewe tukacheki kinachozungumza ili tuweze kuelewana. Malipo ambayo yamefanyika ni haya ambayo nimeyazungumzia hapa na wako wakulima 10 tu ambao ndio wanaonekana kwamba hawajalipwa mpaka sasa hivi. Majina yao ninayo hapa ambayo mwingine anaitwa Sania, majina mafupi mafupi ambayo huwezi kujua kwamba ukitoa hela zikienda kule zitakuwa zinakwenda kwa nani ndio tatizo tunalo. Majina ninayo hapa nimekuja nayo, nimekuja na faili zima liko hapa. Kwa hilo tatizo huwezi kumpa tu mtu anaitwa Bahati, sasa Bahati ni nani huwezi kupeleka zile hela utakuwa unapoteza hela za Serikali. (Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini pia kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge wako wakulima 165 ambao wanaonekana kwamba walikuwa wanalima katika shamba la katani ambalo lilikuwa ni mali ya Serikali hawa wakasema hivi tunaomba mtupatie viwanja hatuna haja ya hela na nini. Hivi ninavyozungumza hapa nimezungumza na Mkurugenzi Mtendaji asubuhi ya leo na amenithibitishia kwamba kazi hiyo inaendelea na viwanja hivyo vinatolewa. Sasa Mheshimiwa Mbunge anazungumza habari ya watu 720 hili si jambo dogo mimi hapa nalichukua kwa uzito tena nikitoka hapa nakwenda nje kupiga simu. Nitamwambia Mkurugenzi wewe unaniambia habari ya watu 165 Mbunge anasema 720 ili tuweze kukamilisha jambo hili tuweze kukaa na Mbunge tuweze kujua ni nini kinachoendelea. Lakini taarifa ndio hiyo majina ninayo na yale mengine ambayo yamekuja mengine matano nayo tunayafanyia kazi tuhakikishe kwamba wanalipwa. |
||||||