You are using an older version of Internet Explorer.

In order to get the most out of our website, you can get a free update of Internet Explorer.
If you're using a work computer, please contact your IT administrator.

[CLOSE]
  email E-mail this to a friend email Printable version

Supplementary Question

mp Barwany, Salum Khalfan[CUF]

Lindi Mjini Constituency
Session No Question Number To the Ministry of Sector Date Asked
5 104 WORKS Transport/Road 17 November 2011
Mheshimiwa Spika ahsante. Katika Bunge lako Tukufu Waziri wa ujenzi aliahidi kwamba itakapofika mwezi Novemba, 2011kipande cha kilomita sitini kutoka Nyamwage mpaka Somanga kitakuwa kimekamilika na sasa mvua za masika zimeanza na athari hii ya mvua ilianza kuonekana katika kipindi cha mwaka uliopita:

Je, Waziri analiambia nini Bunge hili juu ya tatizo ambalo linakwamisha kumalizika kwa kipande kile takriban sasa ni miaka mitatu?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION #  104  SESSION #  5
mp Answer From Hon.Magufuli, Dr. John Pombe Joseph
WORKS
WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE)

Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Barwany, Mbunge wa Lindi, kama ifuatavyo:-

Pamoja na kwamba, swali la msingi lilihusu Barabara ya Pangani hadi Bagamoyo, yenye jumla ya kilomita 178, swali aliloliuliza Mheshimiwa Mbunge ni la kuhusu Ndundu – Somanga, yenye jumla ya kilomita 56. Ninapenda kumthibitishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, sehemu ile ya Somanga – Ndundu, ambayo inajengwa na Kampuni ya Kharafi, kwa gharama ya shilingi bilioni 60 na mkandarasi anaendelea na kazi, itakamilika kulingana na masharti ya Mkataba. Palikuwa na matatizo kidogo ya fedha, lakini kama wiki mbili zilizopita tulimlipa shilingi bilioni tatu.

Tunapanga wiki ijayo tutamlipa tena fedha zingine kutokana na madai yake. Tatizo la Mradi ule ni kwamba, mwanzoni ulikuwa unafadhiliwa na Benki ya Kuwait, baadaye fedha hazikutolewa na Benki ya Kuwait ikabidi fedha zote za Mkataba zitolewe na Serikali ya Tanzania.
Ninataka kuwahakikishia Wananchi wa Kusini kwamba, barabara hii itakamilika kulingana na masharti ya Mkataba na ninamwagiza mkandarasi afanye kazi kwa juhudi zote, kwa sababu anaendelea kulipwa fedha