| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 8 | 326 | ENERGY AND MINERALS | Energy | 6 August 2012 | ||
| Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini nina maswali ya nyongeza. Mheshimiwa Waziri amezungumzia la umeme wa gesi pamoja na makaa ya mawe. Lakini makaa ya mawe ya Ngaka ambayo yameshaanza kuvunwa bado Serikali haijaweka msisitizo wa kujenga transmission line kutoka Ngaka mpaka Songea, Njombe hadi kufika Mufindi. Je, nini majibu ya Serikali kuhusiana na mradi huo wa ujenzi wa Transmission line? Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri amesema kwamba hawawezi kulipa fidia lakini kwa kuwa watu wengi ambao wamechukua mikopo katika mabenki wanashindwa kufanya marejesho kutokana na kutokuwa na uzalishaji wa kutosha kulingana na miradi yao ilivyokuwa. Kwa nini Serikali isitoe dhamana yaani wa bailout kwa kipindi fulani ili watu waweze kujenga uwezo wa kulipa madeni hayo kwa uhakika? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 326 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba maendeleo ya mipango ya uzalishaji wa umeme kupitia makaa ya mawe ya Mchuchuma, Ngaka na Kiwira yanaendelea vizuri. Tuna matarajio kwamba ifikapo mwaka 2015 tunaweza tukawa tumeshaanza kuzalisha takribani MW 200 kutoka Mgodi wa Kiwira na takribani MW 300 kwa Mchuchuma na Ngaka 120. Hayo ndio matarajio yetu. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumhakikishia kwamba mipango ya ujenzi wa miundombinu itakayokwenda sambamba na uzalishaji huu mpya wa umeme iko mbioni na tuna mradi ambao unaendelea sasa na uko kwenye hatua nzuri ambao tunaanza kujenga line kubwa kutoka Makambako kwenda mpaka Songea. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sambamba na hiyo mipango inaendelea ili kuhakikisha kwamba kabla ya uzalishaji huo haujafikiwa basi tumeshajenga line ya kutosha kuweza kusafirisha umeme huo ambao utazalishwa. Lakini jibu la kipengele cha (b) kwamba mikopo iweze kutolewa, kuna watu wamekopa na wanahitaji kurejesha hapa nafikiri swali la msingi lilikuwa limejikita kwenye suala zima la watu waliopoteza ajira. Sasa kama kuna watu ambao wamekopa mikopo na wanahitaji kufanya marejesho kupitia tatizo hili la umeme kwamba wanapata shida, basi hili ni jambo ambalo nafikiri kimsingi ni lazima sisi kama Serikali tuliangalie. Lakini lina namna nyingi ya kuweza kuliangalia, si namna peke yake tu ya kuangalia katika Wizara ya Nishati na Madini kwa maana ya kulipa fidia kupitia kwenye Wizara yetu. Mheshimiwa Spika, lakini niseme tu kwamba, tatizo hili ni la Kitaifa na wote tunafahamu sababu zilizotupelekea kufikia kwenye hatua hii ni kuamini kwamba vyanzo vya maji vingeendelea kuwepo. Lakini sasa Serikali imejikita katika suala zima la kuhakikisha tunaanzisha vyanzo vingine vya kuzalisha umeme kwa njia nyingine kama jua, makaa ya mawe, gesi ambayo inatusaidia sana na hivi tunashukuru Mungu kwamba, tunaendelea kugundua gesi kwa kiasi kikubwa katika exploration zinazoendelea. |
||||||