| E-mail this to a friend | Printable version |
| Session No | Question Number | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
|---|---|---|---|---|---|---|
| 10 | 1 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 29 January 2013 | ||
| Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Ningependa kumwuliza Mheshimiwa Waziri kama ifutavyo:- Maeneo mengi katika Majimbo ya Kilwa Kaskazini na hapa nchini, Wananchi wamekuwa wakifanya jitihada za kujenga majengo na kuyakamilisha, lakini vifaa tiba na wahudumu wa afya ni matatizo kama ilivyo katika eneo la Zinga, Miumbu na Nambondo. Nini mkakati wa Serikali kupeleka vifaa tiba, Wahudumu wa Afya na Waganga katika hospitali hizi ili jitihada zilizofanywa na Wananchi zizae matunda waliyokusudia? |
||||||
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 1 SESSION # 10 | ||||||
|
||||||
| NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mangungu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa tunayo matatizo anayoyasema na kwamba, demand sasa inaonekana ni kubwa, kwa hiyo tunahitaji Madaktari zaidi, tunahitaji Wauguzi zaidi na hivi vifaa tiba pia tunavihitaji. Kwa kuanzia, ambacho kimefanyika sasa hivi, sisi tunafanya kazi na Wizara ya Afya, wapo wanasikia nikijibu hapa tunashirikiana. Moja ni kwamba, idadi ya wanafunzi ambao wanakwenda katika vyuo vyetu ni kubwa. La pili, tumeweka utaratibu kuwa kutoka sasa badala ya kuwapitishia TAMISEMI hawa Wauguzi na Madaktari, wapelekwe kule katika Halmashauri. Mheshimiwa Spika, mimi nimetoka Mikoani, nimetoka Mpanda, tatizo tulilonalo ni kwamba, watumishi wengi ambao wanapangwa katika maeneo ya pembezoni, unakuta hawaripoti kule. Kwa hiyo, tumeanza kuzungumza kuangalia namna tutakavyoweza kuwahamasisha na kutoa motisha waweze kusaidia katika vituo hivi. Mheshimiwa Spika, la pili, anazungumzia kuhusu vifaa tiba; hivi ni sehemu ya ile habari tunayoita Community Health Fund (CHF). Kazi kubwa ni kusaidia ile ruzuku ya Serikali inayokwenda pale na katika Halmashauri nyingi tulizokwenda, tumekuta hela hizi wala ile Community Health Fund haipo, watu wanakwenda kwa ile inayoitwa papo kwa papo, yaani wanalipwa pale halafu wanatibiwa. Kwa hiyo, tumeihamasisha Halmashauri na Mkakati tunaofanya sasa ni kuhakikisha kuwa, watu wote wanajiunga na Mfuko wa Bima ya Afya. Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kwa kumalizia wanapata shilingi milioni 250 kama mfano, ambapo Serikali inawaongezea kutoka NHIF shilingi 250, unakuta wana milioni 500. Katika mazingira ya namna hiyo, hutegemei tena kwamba, hivi vifaa vitakuwa vinakosekana na rai yetu ni kwamba, sisi sote na Mbunge wa Rombo ananisikia nikisema hivyo, kuwa tunawapongeza Watu wa Rombo kwa kufanya vizuri na hawana matatizo ya namna hii. |
||||||